2023
Bundi na Nyangumi
Mei 2023


“Bundi na Nyangumi,” Rafiki, Mei 2023, 8–9.

Bundi na Nyangumi

Ni jinsi gani michoro ya Dieter ingeweza kuwasaidia wengine?

Hadithi hii imetokea huko Kanada.

Picha
Mvulana akipaka rangi picha ya bundi kwenye karatasi

Dieter alitaka asikilize mkutano mkuu. Alijaribu kuketi kwa utulivu. Alijaribu kusikiliza hotuba. Lakini kuwa na ulemavu katika ukuaji kulifanya iwe vigumu kwake kufokasi. Aligaagaa kwenye kochi. Alicheza na wanasesere wake. Alikimbia pande zote.

Kisha alimwangalia Baba yake. Baba alikuwa ameketi kwa utulivu na akiwasikiliza wazungumzaji. Dieter naye alitaka kuwa kama yeye. Kwa hiyo alileta vitu vyake vya sanaa. Pengine kupaka rangi picha kungemsaidia aketi kwa kutulia.

Wakati akipaka rangi, Dieter alimsikiliza Mzee Jeffrey R. Holland akizungumza. Mzee Holland alisimulia hadithi kuhusu Yesu. Yesu alimtaka Kijana tajiri atoe pesa zake zote awape masikini.*

Dieter alitaka kuwasaidia watu ambao pia hawakuwa na pesa za kutosha. Na alipata wazo.

“Mama, nataka kupaka rangi picha ya bundi,“ Dieter alisema. “Unaweza kuchora moja kwa ajili yangu?”

“Hakika,” Mama alisema. Alimchora bundi.

Dieter alichovya brashi yake ndani ya rangi kiasi. Alipaka rangi mabawa ya yule bundi kwanza. Alifanya baadhi ya manyoya kuwa ya kahawia na baadhi ya manyoya rangi ya chungwa. Alipokuwa akipaka rangi, alisikiliza hotuba zingine. Hata wakati hatuba zote zilipokuwa zimekwisha, Dieter aliendelea kufanya kazi. Alitaka bundi awe na mwonekano kamili.

Mwishowe Dieter alimaliza. Alimwonyesha Mama bundi yule.

“Anaonekana mzuri sana!” Mama alisema. “Tumtundike juu?”

Dieter alitikisa kichwa chake hapana, “nataka kuiuza na nitoe pesa hizo ili niwasaidie watu wasiokuwa na pesa za kutosha. Kama walivyozungumza hilo katika mkutano mkuu.”

Mama alitabasamu. “Acha tuone nini tunaweza kufanya.”

Aliituma picha ile iliyopakwa rangi na Dieter mtandaoni ili kuiuza. Mama aliandika kwamba Dieter alisema atatoa pesa hiyo kwenye kituo cha watu wasio na makazi.

Siku iliyofuata, Dieter na Mama waliangalia tangazo. Dieter hakuweza kuamini! Watu wengi walitaka kununua picha yake. Alifurahi kwamba watu wengi mno walitaka kusaidia.

Mgahawa katika jiji la Dieter uliomba kununua mchoro ule. Walisema wangelipa mara 10 zaidi ya kile Dieter na Mama walichoomba! Maduka mengine walimwomba michoro pia. Dieter alikuwa na kazi zaidi ya kufanya!

Mama alichora wanyama zaidi na Dieter alileta rangi zake. Alimpaka rangi mbweha, simba na nyangumi. Alimpenda nyangumi zaidi. Alimpa jina “Nyangumi Otis.” Duka la biashara ya vyakula karibu na nyumba yake liliununua. Mara nyingine Dieter alipokwenda kwenye duka, aliuona ikining’inia ukutani!

Picha
Mvulana akionesha kwenye mchoro wa nyangumi wakati mama yake akitabasamu

“Tazama Mama!” Dieter alionesha kwenye mchoro.

“Wao!” Mama alisema. “Sasa wakati wowote tunapokuja hapa, tunaweza kukumbuka jinsi vipaji vyako vilivyowasaidia watu.”

Dieter aliona fahari kwamba watu walipenda michoro yake. Lakini alikuwa na furaha zaidi kwamba aliweza kuwasaidia wengine. Alifurahi kuwa alisikiliza wakati wa mkutano mkuu.

Picha
Mvulana akiwa ameshikilia mchoro wa bundi
Picha
PDF ya hadithi

Vielelezo na Natalie Campbell

  • Kutoka “The Greatest Possession,” Liahona, Nov. 2021, 8–10.

Chapisha