“Muhtasari wa Mkutano,” Rafiki, Mei 2023, 5.
Muhtasari wa Mkutano
Tunaamini katika Kristo
Rais Oaks alisema kwamba tunaamini katika Yesu Kristo. Alisoma maandiko mengi kuhusu kile Yesu alichosema wakati wa maisha Yake na Alipowatembelea Wanefi. Tunapaswa kujifunza maneno ya Yesu ili yatuongoze katika maisha yetu.
Hili linanifundisha:
Pamoja na Yesu Tena
Mzee Stevenson alisimulia kuhusu wasichana wawili ambao shangazi yao alikuwa amefariki. Mke wa Mzee Stevenson, Lesa, aliwauliza jinsi walivyokuwa wakihisi. Walihuzunika, lakini walishiriki naye ushuhuda wao. Walijua shangazi yao alikuwa na furaha na angeweza kuwa pamoja na Yesu. Imani katika Yesu Kristo na uzima wa milele hutupatia faraja.
Hili linanifundisha:
Ushuhuda kwenye Basi
Mzee Corbitt alizungumza kuhusu mwanamke aliyezungumza naye kwenye basi. Yule mwanamke alimuuliza kwa nini alimwamini Yesu Kristo. Hakuwa na uhakika wa nini cha kusema. Kisha aliamua kufokasia jambo lililo muhimu zaidi. Alimwambia kwamba tunamuhitaji Yesu ili atusaidie kurudi kwa Baba wa Mbinguni. Sisi pia tunaweza kushiriki shuhuda zetu.
Hili linanifundisha:
Kubeba Mawe
Dada Johnson alishiriki jinsi gani mambo magumu maishani ni kama kubeba begi la mgongoni lililojaa mawe. Tunabeba mawe kwa sababu ya dhambi zetu, ubaya wa watu wengine, na changamoto za maisha. Yesu Kristo hutusaidia tuondoe mawe kwenye mabegi yetu ya mgongoni ikiwa tutamgeukia Yeye. Tunaweza pia kusaidia kupunguza uzito wa mabegi ya mgongoni ya wengine kwa kuwajali kama vile ambavyo Yesu angewajali.
Hili linanifundisha: