2023
Mtu Mmoja Mwenye Shukrani
Mei 2023


“Kichwa cha Habari cha Makala,” Rafiki, Mei 2023, 46–47.

Hadithi za Maandiko

Mtu Mmoja Mwenye Shukrani

Picha
Yesu Kristo akiwa amesimama mbele ya wanaume waliofungwa bendeji

Vielelezo na Apryl Stott

Siku moja Yesu Kristo alikutana na wanaume 10. Walikuwa wagonjwa sana.

Picha
Yesu Kristo akizungumza

Wanaume walimwomba Yesu awaponye. Yesu aliwaambia waende wajionyeshe kwa makuhani.

Picha
Wanaume wakitabasamu baada ya kuponywa

Walipokuwa njiani, wanaume hao waliponywa! Walijua kuwa Yesu amewaponya.

Picha
Mwanaume akiwa amepiga magoti mbele ya Yesu Kristo

Mmoja wa wale wanaume 10 alirudi kwa Yesu. Alipiga magoti miguuni pa Yesu na kumshukuru. Yesu alisema aliponywa kwa sababu alikuwa na imani.

Chapisha