2023
Yesu Alifundisha Hekaluni
Mei 2023


“Yesu Alifundisha Hekaluni,” Rafiki, Mei 2023, 24–25.

Hadithi za Yesu

Yesu Alifundisha Hekaluni

Ondoa ukurasa huu na ukunje katika nusu mbili zinazolingana. Kisha inua picha juu wakati ukisimulia hadithi.

Picha
PDF ya hadithi

Wakati Yesu Kristo alipokuwa na umri wa miaka 12, Alikwenda Yerusalemu pamoja na Mariamu na Yusufu.

Walipokuwa wanarudi nyumbani, Mariamu na Yusufu walitambua kwamba Yesu hakuwa pamoja nao. Walirudi haraka Yerusalemu kumtafuta.

Mariamu na Yusufu walimtafuta na kumtafuta. Hatimaye, walimpata Yesu hekaluni. Alikuwa akiwafundisha watu na kujibu maswali yao. Kila mtu alishangazwa kwa jinsi alivyojua kuhusu injili. Yesu alikuwa akifanya kazi ya Baba wa Mbinguni licha ya kuwa alikuwa mdogo.

Sisi pia tunaweza kusaidia kazi ya Baba wa Mbinguni. Tunaweza kushiriki injili. Tunaweza kujifunza kuhusu hekalu. Mambo haya yatatusaidia tujifunze na tukue kama vile Yesu.

Chapisha