2023
Kumfuata Yesu huko Cape Verde
Mei 2023


“Kumfuta Yesu huko Cape Verde,” Rafiki, Mei 2023, 20–21.

Kumfuata Yesu huko Cape Verde

Kutana na Raissa!

Kuhusu Raissa

Picha
Picha ya msichana akitabasamu

Miaka: 11

Kutoka: Kisiwa cha Santiago, Cape Verde

Lugha: Kireno

Malengo na ndoto: Kuolewa ndani ya hekalu na kuwa na familia yake mwenyewe

Familia: Raissa, Mama, Baba na dada wengine wawili wakubwa

Jinsi Raissa Anavyomfuata Yesu

Picha
Msichana mbele ya hekalu

Alipokuwa na miaka mitano, Raissa na familia yake walikuwa wakitafuta kanisa la kwenda. Mara ya kwanza walipokwenda kwenye Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, walihisi kama wanastahili kuwa pale. Raissa alipenda darasa la Msingi. Familia yake ilibatizwa. Na Raissa alipenda kuwa na jioni ya nyumbani kila wiki.

Raissa alipokuwa na miaka sita, yeye na familia yake waliunganishwa katika hekalu la Recife Brazil.

Hivi karibuni Raissa alikwenda kwenye ufunguzi wa wazi wa hekalu la Praia Cape Verde. “Nilfanya mambo muhimu ili kujitayarisha kwenda hekaluni, kama vile kusali, kwenda kanisani, kujifunza maandiko na kujifunza injili,” anasema.

Baada ya hekalu kuwekwa wakfu, aliweza kufanya ubatizo kwa niaba ya mababu zake waliokufa bila kuijua injili. “Hekalu ni zuri sana,” anasema.

Avipendavyo Raissa

Picha
Jengo la Kanisa, zabibu, maua ya zambarau na kikokotoo na alama za hesabu

Mahali: Jengo la Kanisa

Maandiko: 1 Nefi 3:7

Tunda au mboga: Zabibu

Rangi: Zambarau

Somo shuleni: Hisabati

Picha
PDF ya hadithi

Vielelezo na Melissa Manwill

Chapisha