Shughuli za “Njoo, Unifuate kwa Watoto Wadogo,” Rafiki, Mei. 2023, 49.
Agano Jipya
Shughuli za Njoo, Unifuate kwa ajili ya Watoto Wadogo
Kwa ajili ya Luka 12–17; Yohana 11
Cheza mchezo huu wa kubahatisha wa shukrani na watoto wako wadogo! Tafuta kitu fulani unachokitolea shukrani, lakini usikiseme kwanza ni kitu gani. Orodhesha sababu za kwa nini una shukrani kwa mtu huyo au kitu hicho mpaka mtoto wako abahatishe kwa usahihi. Kisha ni zamu yao!
Kwa ajili ya Mathayo 19–20; Marko 10; Luka 18
Waoneshe watoto wako wadogo picha ya hekalu. Eleza kwamba Baba wa Mbinguni anatutaka tuunganishwe ndani ya mahekalu ili familia zetu ziweze kuwa pamoja milele. Imbeni “Families Can Be Together Forever,” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 188)’
Kwa ajili ya Mathayo 21–23; Marko 11; Luka 19–20; Yohana 12
Tembelea hekalu lililo karibu ukiwa na watoto wako wadogo au waoneshe picha mtandaoni. Shiriki ushuhuda rahisi wa jinsi unavyohisi kuhusu hekalu. Kama mnaweza kutembea kuzunguka viwanja vya hekalu, wasaidie watoto watambue hisia za kupendeza za amani za mahali hapo.
Kwa ajili ya Joseph Smith—Mathayo 1; Mathayo 24–25; Marko 12–13; Luka 21
Wasaidie watoto wako wadogo waseme, “Yesu ananitaka niwatumikie wengine.” Kwa pamoja mfikirieni mtu fulani mnayeweza kumsaidia. Baada ya kumsaidia mtu huyo, uliza jinsi kusaidia kulivyowafanya wahisi.