“Majibu kuhusu Hekalu,” Rafiki, Mei 2023, 38–39.
Majibu kuhusu Hekalu.
Ndani ya hekalu kuko vipi?
Hekalu ni nyumba ya Bwana. Ni safi na nzuri ndani. Kila mmoja anavaa mavazi meupe na anajaribu kuwa mnyenyekevu. Ni mahali pa amani pa kumwabudu Mungu, kujifunza na kuhisi upendo wa Mwokozi kupitia Roho Mtakatifu.
Watu wanafanya nini ndani ya hekalu?
Ndani ya hekalu tunajifunza kuhusu mpango wa Mungu na kufanya maagano pamoja Naye. Tunafanya hivi kwa kushiriki katika ibada kama ubatizo, uthibitisho na kuunganishwa na familia zetu.
“Nitavaaje ninapokwenda hekaluni?
Unapaswa kuvaa nguo zako nzuri kwenda hekaluni. Mara unapokuwa ndani, utabadilisha na kuvaa nguo maalumu ili kufanya ibada. Kwa ajili ya ubatizo, wafanyakazi wa hekaluni watakupa vazi jeupe la kuvaa.
Kibali cha hekaluni ni nini?
Kibali cha hekaluni ni kipande kidogo cha karatasi ambacho kinakuruhusu wewe kuingia hekaluni. Unaweza kukipata kutoka kwa mshiriki wa uaskofu wako au urais wa tawi. Atakuuliza kama unatii amri na kama una ushuhuda. Kama unastahili na uko tayari kuingia hekaluni, atakupa kibali cha hekaluni.
Inamaanisha nini kufanya ubatizo kwa niaba ya wafu?
Ndani ya hekalu, unaweza kubatizwa kwa niaba ya watu waliokufa bila kubatizwa. Utavaa mavazi meupe na kuzamishwa ndani (pasipo chochote kubaki juu) ya maji