“Ufunguzi wa Wazi wa Hekalu,” Rafiki, Mei 2023, 16–17.
Ufunguzi wa Wazi wa Hekalu
Svetan alikuwa na shauku ya kungia ndani ya hekalu!
Hadithi hii imetokea huko Marekani.
Svetan alikuwa na shauku. Familia yake ilikuwa ikihama kutoka Argentina kwenda Marekani. Na sasa hatimaye ukawa muda wa kupanda ndege kubwa!
Svetan alitazama nje ya dirisha wakati ndege ilipopaa. Aliwaza jinsi nyumba yao mpya itakavyokuwa. Kila kitu kitakuwa tofauti. Nyumba mpya. Chumba kipya cha kulala. Ujirani mpya. Na kukutana na marafiki wapya! Svetan alikuwa na shauku.
Svetan pia alijua kwamba nyumba yake mpya ilikuwa karibu na hekalu ambalo ndio kwanza lilikuwa limejengwa. Huko Argentina, hekalu lilikuwa mbali sana. Alikuwa ameliona tu katika picha.
Svetan alimgeukia Mama. “Je unadhani tutaweza kuliona hekalu kutokea angani?”
Mama alitabasamu. “Sidhani.” Lakini tutaliona hivi karibuni”
Svetan alitabasamu pia. Mama na Baba walisema kwamba hekalu lilikuwa bado halijafunguliwa. Lakini karibuni kungekuwa na ufunguzi wa wazi wa Hekalu. Hiyo ilimaanisha watu wangeweza kuingia kuliona kabla halijawekwa wakfu. Na familia ya Svetan ilikuwa inaenda kwenye ufunguzi wa wazi wa hekalu hilo! Asingeweza kungoja kuliona hekalu katika maisha halisi.
Saa chache baadaye, Svetan na familia yake walikuwa kwenye nyumba yao mpya. Kulikuwa na mengi ya kufanya. Svetan alisaidia kufungua maboksi yao na kuifanya nyumba yao ionekane nzuri.
Siku kabla ya ufunguzi wa wazi wa hekalu, waliketi sebuleni kuzungumza.
“Hekalu ni nyumba ya Bwana,” Mama alisema. “Tunapokuwa ndani, lazima tuwe wanyenyekevu. Je, unajua hiyo inamaanisha nini?”
“Kuzungumza kwa ukimya ili tuweze kumsikia Roho Mtakatifu vizuri? Svetan aliuliza.
“Hiyo ni sawa,” Mama alisema. “Tunaweza kujifunza mengi tunapokuwa hekaluni.”
Svetan alikubali kwa kichwa. Alitaka kuwa mnyenyekevu sana ili aweze kumhisi Roho Mtakatifu awapo ndani ya hekalu.
Asubuhi iliyofuata, Svetan aliamka mapema sana. Alivalia nguo zake za Jumapili. Punde muda wa kuondoka ukawadia.
Familia ya Svetan ilifika hekaluni. Watu waliwasaidia kufunika viatu vyao kwa karatasi za plastiki.
“Mama, kwa nini waliweka mifuko hii midogo juu ya miguu yangu? Svetan aliuliza.
“Kwa sababu ndani ya hekalu kila kitu ni kipya na safi. Tunataka kulitunza.”
Mwanamke aliwakaribisha. Alisoma maneno kwenye mlango wa hekalu: “Utakatifu kwa Bwana—Nyumba ya Bwana.”
Svetan alishika mkono wa Mama. Walitembea kuingia ndani. Kila kitu kilikuwa kizuri sana! Pengine hii ilikuwa kama mbinguni kulivyo.
“Tazama!” Svetan alinong’ona. Alionesha kwenye mchoro. “Yule pale ni Yesu!”
Walipomaliza, Svetan alihisi furaha. Alikuwa na shukrani kuweza kuingia ndani ya hekalu. Alitaka kuingia ndani tena atakapokuwa mkubwa.