2023
Shughuli za Njoo, Unifuate
Mei 2023


Shughuli za “Njoo, Unifuate,” Rafiki, Mei 2023, 10–11.

Shughuli za Njoo, Unifuate

Kwa ajili ya jioni ya nyumbani, kujifunza maandiko au kwa ajili ya burudani tu!

Kuonesha Shukrani

mnyororo wa karatasi

Vielelezo na Katy Dockrill

Kwa ajili ya Luka 12–17; Yohana 11

Hadithi: Soma hadithi “Mtu Mmoja Mwenye Shukrani” kwenye ukurasa wa 46. Unawezaje kuonesha shukrani?

Wimbo: “Thanks to Our Father” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 20)

Shughuli Kata vipande 10 vya karatasi. Kwenye kila kipande, andika kitu kimoja ambacho unakitolea shukrani. Funga kamba kuzunguka kila kimoja, na ugundishe miisho pamoja kutengeneza mnyororo. Ning’iniza mnyororo wako wa shukrani mahali ambapo utaweza kuuona kila mara.

Shujaa Mkuu wa Huduma

Mvulana katika mavazi ya shujaa mkuu akiwa amesimama pembeni ya mwanamke mzee mwenye mkongojo

Kwa ajili ya Mathayo 19–20; Marko 10; Luka 18

Hadithi: Yesu Kristo alifundisha kwamba tunapaswa kuwasaidia watu wenye shida (ona Marko 10:17–22). Soma “Bundi na Nyangumi” kwenye ukurasa wa 8 kujifunza jinsi mvulana aitwaye Dieter alivyomfuata Yesu.

Wimbo: “Keep the Commandments” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 146–47)

Shughuli: Nenda kwenye ukurasa wa 12 na uwe shujaa mkuu wa huduma!

Mti Unaosikiliza

Mtoto akichora mkono kwenye karatasi

Kwa ajili ya Mathayo 21–23; Marko 11; Luka 19–20; Yohana 12

Hadithi: Zakayo alitaka kumwona Yesu, lakini umati mkubwa ulimzuia asiweze kumwona. Zakayo alipanda mti ili aweze kumwona na kumsikiliza Yesu vizuri zaidi. (Ona Luka 19:2–8.)

Wimbo: “If I Listen with My Heart” (Muziki kwa ajili ya Watoto, ChurchofJesusChrist.org)

Shughuli: Tengeneza mti wa mkono! Kwenye kipande cha karatasi, chora kufuatisha kiganja na mkono wako. Mkono wako utakuwa shina na vidole vyako vitakuwa matawi. Kuzunguka kila tawi, andika au chora njia unazoweza kumsikiliza Yesu.

Mmisionari Sasa

Watu wanne wakiwa wamekaa katika duara na kunyoosha miguu yao

Kwa ajili ya Joseph Smith—Mathayo 1; Mathayo 24–25; Marko 12–13; Luka 21

Hadithi: Yesu Kristo alisema kwamba kabla ya kuja tena, injili itahubiriwa ulimwenguni kote (ona Joseph Smith—Mathayo 1:31). Tunaweza kusaidia kuwa tayari kwa ajili ya Ujio wa Pili kwa kushiriki injili na wengine.

Wimbo “I Hope They Call Me on a Mission” (Kitabu cha Nyimbo za watoto, 169)

Shughuli: Tengeneza beji yako mwenyewe ya mmisionari! Andika jina lako kwenye kipande cha karatasi na kikate. Nyuma yake, andika jambo moja unaloweza kufanya ili kushiriki injili sasa. Funga kwa pini au bandika beji yako ya jina kwenye shati lako.

Miguu ya Huduma

Kwa ajili ya Mathayo 26; Marko 14; Yohana 13

Hadithi: Yesu Kristo aliosha miguu ya mitume wake (ona Yohana 13:4–16). Aliwapenda na alitaka kuwahudumia. Yesu aliwaambia wafuate mfano Wake na wahudumiane wao kwa wao.

Wimbo: “‘Give,’ Said the Little Stream,” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 236)

Shughuli: Cheza mchezo huu wa huduma. Kila mtu anakaa na miguu yake ikiwa ndani ya duara. Mchezaji mmoja anachagua namba. Wakianzia na miguu yao wenyewe, mchezaji anaonesha kwa kidole kila mguu ndani ya duara na anahesabu kwenda chini kutoka namba ile mpaka wanafika “moja.” Mguu namba “moja” unatoka. Kisha mchezaji yule anachagua namba na anahesabu kwenda chini. Mtu wa mwisho mwenye mguu ndani ya duara anachagua shughuli ya huduma kwa ajili ya kundi kufanya.