“Burudani za Kukunja,” Rafiki, Mei 2023, 32–33.
Kitu cha kuburudisha
Burudani ya Kukunja
Alamisho ya Origami
-
Kunja kipande cha karatasi cha mraba kwa nusu mshazari ili kutengeneza pembe tatu.
-
Kunja pande zote mbili za pembe tatu kwa katikati tengeneza mraba. Kisha kunjua.
-
Shika tabaka la juu la karatasi kwa ncha ya pembe tatu na ikunje kwa kushuka chini.
-
Chomeka miisho ya kulia na kushoto ya pembe tatu ndani ya mfuko.
-
Sasa unaweza kusoma ukiwa na alamisho yako mpya!
Origami ya Mbweha
-
Kunja kipande cha karatasi cha mraba kwa nusu mshazari ili kutengeneza pembe tatu.
-
Kunja upande wa kulia na kushoto wa pembe tatu kwa katikati ili kutengeneza mraba.
-
Geuza mraba upande wa pili. Kunja kwa nusu kupitia mstari wa katikati ili kutengeneza pembe tatu.
-
Tafuta ukingo wa pembe tatu ambao una mikunjo mitatu. Kunja pembe hii juu kwenye mteremko na kisha fungua mikunjo.
-
Fungua mkunjo wa kati na kunja ncha chini ili kutengeneza uso.
-
Chukua ncha nyingine ya pembe tatu kubwa na ikunjie chini kutengeneza mkia.
Origami ya Samaki
-
Kunja kipande cha karatasi cha mraba kwa nusu mshazari kutengeneza pembe tatu, kisha kunjua. Fanya vivyo hivyo kwenye upande mwingine.
-
Kunja karatasi katika pande mbili zinazolingana kutengeneza mstatili, kisha kunjua.
-
Geuza karatasi yako upande wa pili. Finya mikunjo ya kila kona ya mshazari kwenye kingo. Lete kona mbili za kulia pamoja mpaka kingo ziwe sawa. Fanya hivyo hivyo kwenye upande wa kushoto. Unapaswa kuwa na umbo la pembe tatu.
-
Kunja mkunjo mmoja kuelekea katikati. Kunja mkunjo mwingine juu ya ule wa kwanza Hii itatengeneza mapezi.
-
Sasa mgeuze samaki wako na chora jicho.