“Salamu kutoka Cape Verde!” Rafiki, Mei 2023, 22–22
Salamu kutoka Cape Verde!
Jifunze kuhusu watoto wa Baba wa Mbinguni ulimwenguni kote.
Cape Verde ni nchi ya kisiwa iliyo karibu na pwani ya Afrika Magharibi. Takribani watu 480 elfu wanaishi huko.
Lugha
Kireno ni lugha rasmi. Watu pia wanazungumza Krioli ya Cape Verde, au Kikriolu, ambacho kinatokana na Kireno.
Volkano
Cape Verde ina visiwa 10, ambavyo vilitengenezwa kutokana na volkano. Volkano kubwa ambayo iko hai inaitwa Pico do Fogo. Ina urefu upatao futi 9,281 (mita 2,829)
Dini
Takribani asilimia 80 ya watu ni Wakatoliki. Pia kuna takribani waumini elfu 16 wa Kanisa letu.
Muziki
Watu wa Cape Verde wanapenda muziki! Kwa kawaida wanaimba kwa Kikrioli, na muziki wao unachanganya staili kutoka Ureno, Brazil na Afrika Magharibi
Hekalu la Praia
Hekalu la kwanza la Cape Verde liliwekwa wakfu mwaka uliopita!