2023
Kuwa Mpatanishi
Mei 2023


Ujumbe wa Mkutano kutoka kwa Nabii

Kuwa Mpatanishi

Imetoholewa kutoka, “Wapatanishi Wanahitajika,” Liahona, Mei 2023

Kama wafuasi wa Yesu Kristo, tunapaswa kuwa mifano ya jinsi ya kuchangamana na wengine. Njia mojawapo iliyo rahisi zaidi ya kumtambua mfuasi wa kweli wa Yesu Kristo ni jinsi gani mtu huyo anavyowatendea watu wengine kwa huruma.

Mwokozi aliliweka hili wazi. “Heri wapatanishi,” Alisema (Mathayo 5:9; ona pia 3 Nefi 12:9). Wafuasi Wake wa kweli hujenga, huinua, huhamasisha, na kutia moyo—bila kujali ugumu wa hali. Wafuasi wa kweli wa Yesu Kristo ni wapatanishi.

Jinsi tunavyotendeana ndicho cha muhimu zaidi! Jinsi tunavyozungumza na wengine na kuhusu wengine nyumbani, kanisani, na mtandaoni ni muhimu sana. Tunaweza kuubadili ulimwengu—mtu mmoja na mchangamano mmoja kwa wakati mmoja.

Tofauti ni sehemu ya maisha. Acha tuoneshe kwamba kuna njia ya heshima ya kutatua kutoelewana. Omba ili upate ujasiri na hekima ya kusema na kufanya kile ambacho Mwokozi angefanya.

Ninawasihi mchague kuwa wapatanishi, sasa na daima.

Picha
Alt text

“Alifungua Kinywa Chake na Kuwafundisha” na Michael Malm

Tunaweza Kuubadili Ulimwengu

Rais Nelson alisema kwamba kile tunachofanya na kusema ni muhimu sana! Katika nafasi zilizo hapa chini, andika kile unachoweza kusema ili kusaidia kuleta amani.

Je, unaweza kusema nini kwa mtu mwenye huzuni?

Je, unaweza kusema nini wakati mtu anapochukua vitu vyako?

Je, unaweza kusema nini wakati mtu anapokuonea?

Picha
alt text here

Chapisha