2010–2019
Ujumbe, Maana, na Umati
Mkutano Mkuu wa Oktoba 2019


Ujumbe, Maana, na Umati

Katika makelele yasiyokoma ya siku zetu, na tujitahidi kumuona Kristo kwenye kiini cha maisha yetu, imani yetu, na huduma yetu.

Akina kaka na akina dada, huyu ni Sammy Ho Ching, mwenye miezi saba, akitazama mkutano mkuu kwenye televisheni nyumbani kwao Aprili iliyopita.

Picha
Sammy Ho Ching akitazama mkutano

Wakati muda ulipokaribia wa kumuidhinisha Rais Russell M. Nelson na Viongozi wengine Wakuu Wenye Mamlaka, mikono ya Sammy ilikuwa ikishikilia chupa yake. Kwa hivyo alifanya kitu kizuri zaidi alichoweza.

Picha
Sammy Ho Ching wakati wa kuidhinisha

Sammy analeta maana mpya kabisa kwenye wazo la kura ya kuidhinisha kwa kutumia miguu yako.

Karibuni kwenye mkutano huu wa nusu mwaka wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Ili kuweka mazingira ya majadiliano yangu kuhusu maana ya mikutano hii ya mara mbili kila mwaka, ninachukua mazingira haya kutoka simulizi ya Luka katika Agano Jipya:1

“Ikawa [Yesu] alipokaribia Yeriko, mtu mmoja kipofu alikuwa ameketi kando ya njia, akiomba sadaka:

“… Alipowasikia makutano wakipita, aliuliza, kuna nini.

“… Wakamwambia, Yesu wa Nazareti anapita.

“Akapiga kelele, akisema, Yesu, Mwana wa Daudi, unirehemu.”

Wakiwa wameshtushwa na ujasiri wake, umati ulijaribu kumnyamazisha mwanaume yule, lakini “yeye alizidi sana kupaza sauti,” inasemekana. Kwa sababu ya kushikilia msimamo wake, aliletwa kwa Yesu, ambaye alisikiliza ombi lake la imani kwa ajili ya kurudishiwa uwezo wake wa kuona na akamponya.2

Nasisimka kutokana na hadithi hii kila niisomapo. Tunaweza kuhisi dhiki ya mwanaume huyu. Tunaweza kumsikia kwa kiasi fulani akipaza sauti kwa ajili ya usikivu wa Mwokozi. Tunatabasamu kwa sababu ya kukataa kwake kunyamazishwa—naam, azimio lake la kupaza sauti juu wakati kila mtu alipokuwa akimtaka anyamaze kimya. Hakika, ndani yake na yenyewe, ni hadithi nzuri ya imani imara. Lakini sawa na maandiko yote, kadiri mara nyingi tunavyozidi kuisoma, ndivyo tunavyopata zaidi kutoka ndani yake.

Wazo moja lililonijia hivi karibuni ni uwezo mzuri wa kuhisi aliokuwa nao mtu huyu katika kuwa na watu wenye hisia za kiroho kumzunguka. Umuhimu wote wa hadithi hii unabebwa katika wanawake na wanaume wachache wasiojulikana ambao, wakati walipoulizwa na wenzao, “Ni nini maana ya vurumai hii?” walikuwa na ono, kama utasema hivyo, la kumtambua Kristo kama sababu ya kelele; Alikuwa Mfano Halisi wa Maana. Kuna somo kwa kila mmoja wetu katika mazungumzo haya. Katika maswala ya imani na kusadikisha, inasaidia kuelekeza maswali yako kwa wale ambao wanayo baadhi ya maswali! “Je! Aliye kipofu aweza kumuongoza kipofu?” Yesu wakati mmoja aliuliza. “[Kama ni hivyo,] hawatatumbukia shimoni wote wawili?”3

Kutafuta imani kama huku na kusadikisha ndilo lengo letu katika mikutano hii, na kwa kuungana nasi leo, utagundua ya kwamba kutafuta huku ni jitihada inayofanywa na wengi. Tazama karibu nawe. Hapa katika bustani hii unaona familia zenye ukubwa wa aina zote zikija kutoka pande zote. Marafiki wa zamani hukumbatiana kwa kukutana kwa furaha, kwaya ya kupendeza inajiandaa, na wapinzani wanapiga kelele kutoka kwenye kikwezeo chao wanachokipenda. Wamisionari wa zamani wakitafuta waliotumikia nao zamani, wakati wale walirudi toka misheni hivi karibuni wakitafuta wenza wapya kabisa (kama unafahamu ninachomaanisha!). Na picha? Mbingu itusaidie! Na simu za mkononi katika kila mkono, tumebadilika kutoka “kila muumini mmisionari” kuwa “kila muumini mpiga picha.” Katikati ya vurumai hii ya kupendeza, mtu angeweza kuuliza, “Ni nini maana ya yote haya?”

Kama katika hadithi yetu ya Agano Jipya, wale waliobarikiwa na uwezo wa kuona watatambua hilo, licha ya kila kitu kingine ambacho desturi ya mkutano huu inaweza kutoa, itakuwa haina maana sana au isiyo na maana isipokuwa tumpate Yesu katika kiini cha yote haya. Kuelewa maono tunayotafuta, uponyaji Anaoahidi, umuhimu ambao kwa kiasi fulani tunajua uko hapa, lazima tushinde vurumai—hata iwe ya kufurahisha kiasi gani—na kufokasi umakini wetu Kwake. Sala ya kila mnenaji, matumaini ya wote wanaoimba, staha ya kila mgeni—vyote vimekusudiwa kumualika Roho wa Yule ambaye hili ni Kanisa Lake—Kristo anayeishi, Mwanakondoo wa Mungu, Mfalme wa Amani.

Lakini hatutakiwi kuwa katika kituo cha mkutano ili tuweze Kumpata. Wakati mtoto anaposoma Kitabu cha Mormoni kwa mara ya kwanza na kuvutiwa na ujasiri wa Abinadi au kutembea kwa askari mashujaa 2,000, tunaweza kuongeza kwa upole kwamba Yesu ndiye mkuu kwa sasa aliye katika kumbukumbu hii ya kupendeza akisimama kama mwenye umuhimu mkubwa kwenye karibia kila ukurasa na akitoa kiunganishi kwa vitu vingine vyote vya kuleta imani vilivyomo ndani yake.

Kadhalika, wakati rafiki anapojifunza kuhusu imani yetu, anaweza kushindwa na baadhi ya vipengele vya kipekee na msamiati usiojulikana sana wa desturi yetu ya kidini—vizuizi kuhusu vyakula, vifaa vya kujitegemea, safari za waanzilishi, historia ya familia ya kidijitali, pamoja na idadi kubwa ya vituo vya vigingi ambapo bila shaka baadhi wametarajia kuhudumiwa chakula. Kwa hivyo, wakati rafiki zetu wapya wanapopata uzoefu wa mazingira mapya, ni lazima tuoneshe mbele zaidi kwa kusonga kwa bidii na kuwakita zaidi katika maana ya haya yote, katika moyo wenye uhai wa injili ya milele—upendo wa Wazazi wa mbinguni, zawadi ya Upatanisho ya Mwana mtukufu, Mwongozo wenye faraja wa Roho Mtakatifu, urejesho wa siku za mwisho wa kweli hizi zote na zaidi.

Wakati mtu anapokwenda katika hekalu takatifu kwa mara ya kwanza, anaweza kuingiwa na hofu na tukio hilo. Jukumu letu ni kuhakikisha kwamba ishara takatifu na ibada zilizofunuliwa, mavazi maalum na mawasilisho ya kuonekana, kamwe havitutoi kutoka kwa Mwokozi badala yake vinatuelekeza kwa Mwokozi, ambaye tuko pale kumuabudu. Hekalu ni nyumba Yake, na Yeye lazima atawale katika akili na mioyo yetu—mafundisho matukufu ya Kristo yaliyoenea katika nafsi yetu kama yanavyoenea katika ibada za hekaluni—kuanzia wakati tunaposoma maandishi yaliyo juu ya mlango wa mbele mpaka muda wa mwisho tunapokuwa ndani ya jengo. Katikati ya mshangao tunaopata, tunapaswa kuona, zaidi ya mengine yote, maana ya Yesu katika hekalu.

Fikiria muunganiko wa matukio na matangazo mapya Kanisani katika miezi hii ya karibuni. Tunapohudumiana, au tunapoboresha uzoefu wetu wa Sabato, au tunapokubali mpango mpya kwa ajili ya watoto na vijana, tutakosa sababu halisi ya marekebisho haya yaliyofunuliwa ikiwa tutayaona kama ya utofauti kabisa, vipengele visivyohusiana badala ya kama juhudi zinazoshabihiana kutusaidia kujenga juu ya Mwamba wa Wokovu wetu.4 Hakika, hakika, hili ndilo Rais Russell M. Nelson anakusudia kwa kututaka tutumie jina lililofunuliwa la Kanisa.5 Kama Yesu—Jina Lake, Mafundisho Yake, Mfano Wake, Utukufu Wake—vinaweza kuwa kiini cha kuabudu kwetu, tutakuwa tunaimarisha ukweli ambao Alma alifundisha wakati fulani: “Kuna vitu vingi vitakavyokuja; [lakini] tazama, kuna kitu kimoja ambacho ni muhimu kuliko vyote— … Mkombozi [ambaye] ataishi miongoni mwa watu Wake.”6

Wazo moja la kuhitimisha: Mandhari ya uanzilishi ya Joseph Smith katika Karne ya 19 yalikuwa yamejawa na umati wa mashahidi wa Kikristo walioshindana.7 Lakini katika ghasia waliyosababisha, hawa viongozi wachangamfu walikuwa, kwa kejeli, wakimzuia Mwokozi yule yule ambaye Joseph mdogo alikuwa akimtafuta. Akipigana na kile alichokiita “giza na mchafuko,”8 alijiondoa kwa muda na kwenda mahali pa upweke kwenye kijisitu ambapo aliona na kusikia ushahidi mtukufu zaidi wa uhalisia wa Mwokozi kwenye injili kuliko chochote tulichotaja hapa asubuhi hii. Akiwa na karama ya kuona isiyofikirika na kutarajiwa, Joseph alimuona katika ono Baba Yake wa Mbinguni, Mungu mkuu wa ulimwengu, na Yesu Kristo, Mwanawe Pekee mkamilifu. Kisha Baba alitoa mfano ambao tumekuwa tukiushangilia asubuhi ya leo: Alimwonyesha Yesu, akisema: “Huyu ni Mwanangu Mpendwa. Msikilize Yeye!”9 Hakuna onyesho kubwa zaidi la utambulisho mtukufu wa Yesu, umuhimu Wake katika mpango wa Wokovu, na hadhi Yake mbele za Mungu vinaweza kuzidi tangazo lile fupi la maneno saba.

Vurumai na kiwewe? Umati na ushindani? Kuna wingi wa hayo katika ulimwengu wetu. Hakika, wenye kushuku na waaminifu wangali wanashindana juu ya ono hili na karibu kila kitu nilichorejelea leo hii. Iwapo wewe unaweza kuwa ukijitahidi kuona vizuri zaidi na kutafuta maana katikati ya maoni mengi, ninakuelekeza kwa Yesu yuleyule na ninatoa ushahidi wa kitume juu ya uzoefu wa Joseph Smith, ukija kama ulivyokuja takriban miaka 1,800 baada ya rafiki yetu kipofu kupokea uoni wake kwenye Barabara ya kale ya Yeriko. Ninashuhudia pamoja na hawa wawili na wengine wengi kwamba uoni na sauti ya kupendeza katika maisha ni ile ya Yesu si tu akipita10 bali ujio Wake kwetu , akisimama kando yetu, na kufanya makao pamoja nasi.11

Akina dada na akina kaka, katika makelele yasiyokoma ya siku zetu, na tujitahidi kumuona Kristo katika kiini cha maisha yetu, imani yetu, na huduma yetu. Hapo ndipo maana ya kweli ilipo. Na kama baadhi ya siku uwezo wetu wa kuona utazuiliwa, au ujasiri wetu utafifia au uaminifu wetu unajaribiwa na kutakaswa—kwani hakika itakuwa hivyo —na tupaze sauti zetu, “Yesu, Mwana wa Daudi, unirehemu.”12 Ninaahidi kwa ari ya kitume na imani ya kinabii kwamba atakusikiliza na atasema, sasa au baadaye, “Upate kuona: imani yako imekuponya.”13 Karibuni kwenye mkutano mkuu Katika Jina la Yesu Kristo, amina.

Chapisha