Kuwa wa Maagano
Kuwa wa Mungu na kutembea pamoja na kila mmoja kwenye njia Yake ya maagano ni kubarikiwa kupitia kuwa wa maagano.
Wapendwa kaka zangu na dada zangu, hadithi inasimuliwa ya mtoto wa msingi anayejifunza kusali. “Asante kwa herufi A, herufi B, … herufi G.” Sala ya mtoto inaendelea, “Asante kwa herufi X, Y, Z. Baba mpendwa wa Mbinguni, asante kwa nambari 1, nambari 2.” Mwalimu wa Msingi ana wasiwasi lakini anasubiri. Mtoto anasema, “Asante kwa nambari 5, nambari 6—na asante kwa mwalimu wangu wa Msingi. Ni yeye pekee ambaye amewahi kuniruhusu nikamilishe sala yangu.”
Baba wa Mbinguni husikia sala ya kila mtoto. Kwa upendo usio na kikomo, Anatuita tuje tuamini na tuwe sehemu kupitia agano.
Dunia hii imejaa mazigazi, njozi, kiini macho. Mengi yanaonekana ya kupita na ya juujuu. Wakati tunapovua vinyago, kujifanya kwetu, kutaka sifa au kutotaka sifa za watu, tunatafuta zaidi ya uzuri wa bandia, uhusiano wa kupita, au kutafuta kwa uchoyo vitu vya kidunia. Uzuri, kuna njia ya kutatua suala hilo.
Tunapofuata amri kuu za Mungu kumpenda Yeye na wale wanaotuzunguka kupitia agano, tunafanya hivyo si kama mgeni lakini kama mtoto Wake nyumbani.1 Msemo wa kale bado ni wa kweli. Katika kujikana nafsi zetu za kidunia kupitia maagano, tunapata na kuwa nafsi bora zaidi ya milele2—huru, hai, halisi—na kufafanua mahusiano yetu ya muhimu zaidi. Kuwa wa Maagano ni kufanya na kutunza ahadi takatifu kwa Mungu na kwa sisi kwa sisi kupitia ibada takatifu ambazo zinaalika nguvu za kiungu zionekane katika maisha yetu.3 Tunapoweka maagano katika hali yote, tunakuwa zaidi ya tulivyo. Kuwa wa maagano kunatupatia mahali, maelezo, na uwezo wa kuwa. Kunaleta imani iletayo uzima na ukombozi.4
Maagano matakatifu huwa chanzo cha upendo kwa ajili ya na kutoka kwa Mungu na kutokea hapo huwa kwa ajili ya na kwetu sisi kwa sisi. Mungu, Baba yetu wa Mbinguni, anatupenda zaidi na anatujua kuliko tunavyojipenda au kujijua. Imani katika Yesu Kristo na mabadiliko binafsi (toba) yanaleta rehema, neema, msamaha. Hivi hufariji maumivu, upweke, udhalimu tunaopitia katika maisha haya. Kama Mungu, Baba yetu wa Mbinguni anataka tupokee kipawa kikuu cha Mungu—shangwe Yake, uzima Wake wa milele.5
Mungu Wetu ni Mungu wa maagano. Kwa asili yake, Yeye “huyashika maagano na kuonyesha rehema.”6 Maagano yake yanadumu, “kadiri muda [utakapokuwepo], au dunia itakapokuwepo, au [kutakuwa] na mtu mmoja juu ya uso wake kuokolewa.”7 Hatujakusudiwa kutangatanga katika shaka na wasiwasi lakini kufurahia katika mahusiano pendwa ya maagano “imara zaidi kuliko kamba za mauti.”8
Ibada na maagano ya Mungu yana mahitaji sawa kwa wote na ni binafsi katika fursa zake. Kupitia usawa alio nao Mungu, kila mtu katika kila sehemu na umri anaweza kupokea ibada okozi. Haki ya kujiamulia hutumika—watu huamua ikiwa watachagua ibada zitolewazo. Ibada za Mungu hutoa vibao elekezi katika njia Yake ya maagano. Tunauita mpango wa Mungu kuwaleta watoto Wake nyumbani mpango wa ukombozi, mpango wa wokovu, mpango wa furaha. Ukombozi, wokovu, furaha ya selestia vinawezekana kwa sababu Yesu Kristo “alikamilisha upatanisho huu mkamilifu.”9
Kuwa wa Mungu na kutembea pamoja na kila mmoja kwenye njia Yake ya maagano ni kubarikiwa kupitia kuwa wa maagano.
Kwanza, kuwa wa Maagano kuna kiini katika Yesu Kristo kama “mpatanishi wa agano jipya.”10 Mambo yote yanaweza kufanya kazi kwa pamoja kwa faida yetu wakati “tumetakaswa katika Kristo … katika agano la Baba.”11 Kila baraka nzuri na iliyoahidiwa huja kwa wale wanaovumilia kwa uaminifu hadi mwisho. “Hali ya furaha ya wale wanaotii amri za Mungu” ni “kubarikiwa katika vitu vyote, vya muda na vya kiroho,” na “kuishi na Mungu katika … furaha isiyo na mwisho.”12
Tunapoheshimu maagano yetu, wakati mwingine tunaweza kuhisi tuko pamoja na malaika. Na tutakuwa—wale tunaowapenda na kutubariki upande huu wa pazia na wale wanaotupenda na kutubariki upande mwingine wa pazia.
Hivi karibuni mimi na Dada Gong tuliona hali ya kuwa wa maagano kwenye uzuri wake wa kupendeza katika chumba cha hospitali. Baba kijana alihitaji upandikizaji wa dharura wa figo. Familia yake ilikuwa imelia, imefunga, na kusali kwa niaba yake aweze kupata figo. Wakati habari ilipokuja kwamba figo ya kuokoa maisha ilikuwa imepatikana, mkewe kwa utulivu alisema, “Natumaini hiyo familia nyingine iko SAWA.” Kuwa wa maagano ni, katika maneno ya Mtume Paulo, “tufarijiane mimi na ninyi, kila mtu kwa imani ya mwenzake, yenu na yangu.”13
Katika njia ya maisha, twaweza kupoteza imani katika Mungu, lakini kamwe Yeye hapotezi imani kwetu sisi. Kama ilivyokuwa, taa Yake ya ukumbini siku zote inawaka. Anatualika twende au turudi kwenye maagano ambayo yanaonesha njia Yake. Anasubiri kwa utayari kutukumbatia, hata wakati “tunapokuwa tungali mbali.”14 Tunapotazama kwa jicho la imani mfumo, tao, au nukta zilizounganishwa za uzoefu wetu, tunaweza kuona neema Yake ya huruma na tumaini, hasa katika majaribu, huzuni, na changamoto, na vile vile katika furaha yetu. Bila kujali ni mara ngapi tunajikwaa au kuanguka, kama tutaendelea kusonga kuelekea Kwake, Yeye atatusaidia, hatua kwa hatua.
Pili, Kitabu cha Mormoni ni ushahidi ambao tunaweza kuubeba kwenye mkono wetu wa kuwa wa maagano. Kitabu cha Mormoni ni kifaa kilichoahidiwa kwa ajili ya kuwakusanya watoto wa Mungu, kilichotolewa unabii kama agano jipya.15 Tunaposoma Kitabu cha Mormoni, sisi wenyewe pamoja na wengine, iwe ni kimya kimya au kwa sauti, tunaweza kumuuliza Mungu “kwa moyo wa kweli, na kusudi halisi tukiwa na imani katika Kristo,” na kupokea kupitia nguvu ya Roho Mtakatifu uthibitisho wa Mungu kuwa Kitabu cha Mormoni ni cha kweli.16 Hii hujumuisha hakikisho kwamba Yesu Kristo ni Mwokozi wetu, Joseph Smith ni Nabii wa Urejesho, na Kanisa la Bwana linaitwa kwa jina Lake—Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho.17
Kitabu cha Mormoni huzungumza kupitia agano la kale na jipya kwenu ninyi mlio watoto wa Lehi, “watoto wa manabii.”18 Mababu zenu walipokea ahadi ya agano kwamba nyinyi, uzao wao, mngetambua sauti kama iliyotoka mavumbini katika Kitabu cha Mormoni.19 Hiyo sauti mnayoihisi mnaposoma inashuhudia ninyi ni “watoto wa agano”20 na Yesu ni Mchungaji wenu Mwema.
Kitabu cha Mormoni kinatualika kila mmoja wetu, kwa maneno ya Alma, tuingie “kwenye agano na [Bwana], kwamba [sisi] tutamtumikia na kushika amri zake, ili atuteremshie Roho yake juu [yetu] zaidi.”21 Wakati tunapotaka kubadilika kwa wema—jinsi mtu mmoja alivyosema, “kuacha kuteseka na kufurahia kuwa na furaha”—tunaweza kuwa radhi kuongozwa, kusaidiwa, na kutiwa nguvu. Tunaweza kuja kupitia agano kuwa pamoja na Mungu na jumuiya ya waumini waaminifu na kupokea baraka zilizoahidiwa katika mafundisho ya Kristo22—hivi sasa.
Mamlaka ya ukuhani yaliorejeshwa na nguvu ya kubariki watoto Wake wote ni kipimo cha tatu cha kuwa wa maagano. Katika kipindi hiki, Yohana mbatizaji na Mitume Petro, Yakobo, na Yohana wamekuja kama wajumbe waliotukuzwa kutoka kwa Mungu ili kurejesha mamlaka Yake ya ukuhani.23 Ukuhani wa Mungu na ibada Zake zinafanya mahusiano duniani kuwa matamu na unaweza kuunganisha mahusiano ya agano mbinguni.24
Ukuhani unaweza kubariki kihalisia toka kuzaliwa hadi kifo—toka jina la mtoto mchanga hadi kuweka kaburi wakfu. Baraka za ukuhani huponya, hufariji, hushauri. Baba alikuwa amekasirishwa na mwanawe, mpaka hisia za upendo za msamaha zilipokuja wakati baba alipompa mwanaye baraka ya ukuhani. Muumini pekee katika familia yake, msichana mpendwa alikuwa hana hakika kuhusu upendo wa Mungu kwake mpaka wakati alipopokea baraka ya ukuhani. Kote ulimwenguni, baba wakuu waadilifu hujiandaa kiroho kwa ajili ya kutoa baraka za baba mkuu. Wakati baba mkuu anapoweka mikono yake juu ya kichwa chako, anahisi na kuonesha upendo wa Mungu kwako. Anataja ukoo wako katika nyumba ya Israeli. Anataja baraka kutoka kwa Bwana. Kama wazo, mke wa baba mkuu mmoja aliniambia jinsi yeye na familia yake wanavyomualika Roho, hasa katika siku ambazo baba hutoa baraka za baba mkuu.
Hatimaye, baraka za kuwa wa maagano huja wakati tunapomfuata nabii wa Mungu na kufurahia katika kuishi maagano ya hekaluni, ikiwa ni pamoja na ndoa. Maagano ya ndoa huwa ya kiungu na ya milele wakati tunapochagua kila siku furaha ya mwenza na familia zetu kabla ya ile ya kwetu. Wakati “mimi” inapokuwa “sisi,” tunakua pamoja. Tunazeeka pamoja; tunakua vijana pamoja. Tunapobarikiana sisi kwa sisi katika maisha ya kutojijali nafsi zetu, tunapata matumaini na furaha yetu vimetakaswa katika maisha haya na ya milele.
Wakati hali hutofautiana, wakati tunapofanya yote tuwezayo, vizuri kadiri tuwezavyo, na kwa moyo wa dhati kuomba na kutafuta msaada Wake kote njiani, Bwana atatuongoza, katika muda na namna Yake, kupitia Roho Mtakatifu.25 Maagano ya ndoa yanafungwa kupitia uchaguzi wa wote wawili wanaoyafanya—ukumbusho wa heshima ya Mungu na ya kwetu juu ya haki ya kujiamulia na baraka ya msaada Wake wakati kwa umoja tunautafuta.
Matunda ya kuwa wa maagano katika vizazi vya familia yanaonekana katika nyumba zetu na mioyo yetu. Tafadhali niruhusuni nielezee kupitia mfano binafsi.
Wakati mimi na Dada Gong tulipokuwa tunapendana kuelekea kuoana, nilijifunza kuhusu haki ya kujiamulia na maamuzi. Kwa muda fulani, tulikuwa tunasoma katika nchi mbili tofauti na katika mabara mawili tofauti. Hii ndiyo sababu naweza kusema kwa uwazi kwamba nilipata shahada ya uzamivu katika mahusiano ya kimataifa.
Nilipouliza, “Baba wa Mbinguni, je, nimuoe Susan?” Nilihisi amani. Lakini ilikuwa ni wakati nilipojifunza kuomba kwa kusudi halisi, “Baba wa Mbinguni, nampenda Susan na nataka kumuoa. Naahidi nitakuwa mume na baba mzuri ninayeweza kuwa”—nilipotenda na kufanya maamuzi yangu sahihi, ndipo hapo uthibitisho wangu wenye nguvu ulipokuja.
Sasa chati zetu za kumbukumbu za familia za Gong na Lindsay, hadithi, na picha hutusaidia kugundua na kuungana kupitia uzoefu wa kizazi cha kuwa wa maagano.26 Kwetu sisi, mababu walioheshimika ni pamoja na:
Bibi-Mkuu Alice Blauer Bangerter, ambaye alipata mapendekezo matatu ya ndoa ndani ya siku moja, baadae alimuomba mume wake kuweka pedali kwenye gudulia lake la siagi ili aweze kutengeneza siagi, kufuma, na kusoma kwa wakati mmoja.
Babu-Mkuu Loy Kuei Char aliwabeba watoto wake mgongoni na mali kidogo ya familia yake juu ya punda walipokuwa wakivuka mashamba ya lava kwenye Kisiwa Kikubwa cha Hawaii. Kujitolea na dhabihu za vizazi vya familia ya Char vinabariki familia yetu leo hii.
Gram Mary Alice Powell Lindsay aliachwa na watoto watano wadogo wakati mumewe na mwanawe mkubwa wote wawili walipoaga dunia ghafla katika kipindi cha siku chache. Mjane kwa miaka 47, Gram alilea familia yake kwa upendo wa kuhimili kutoka kwa viongozi na waumini wa eneo lake. Kipindi hicho cha miaka mingi, Gram alimuahidi Bwana kwamba kama angemsaidia, asingelalamika kamwe. Bwana alimsaidia. Hakulalamika kamwe.
Wapendwa akina kaka na akina dada, kama ilivyoshuhudiwa na Roho Mtakatifu, kila kitu chema na cha milele kinalenga katika uhalisia hai wa Mungu, Baba yetu wa Milele, na Mwanaye, Yesu Kristo, na Upatanisho Wake. Bwana wetu, Yesu Kristo, ndiye Mpatanishi wa agano jipya. Kushuhudia juu ya Yesu Kristo ni lengo la agano la Kitabu cha Mormoni.27 Kupitia kiapo na agano, mamlaka ya ukuhani wa Mungu yaliyorejeshwa yamedhamiriwa kubariki watoto wote wa Mungu, ikijumuisha kupitia maagano ya ndoa, vizazi vya familia, na baraka binafsi.
Mwokozi wetu anatangaza, “Mimi ni Alfa na Omega, Kristo Bwana; ndiyo, Mimi ndiye, mwanzo na mwisho, Mkombozi wa ulimwengu.”28
Pamoja nasi toka mwanzo, Yeye Yuko nasi, katika kuwa kwetu wa maagano, mpaka mwisho. Ninashuhudua hivyo katika jina tukufu na takatifu la Yesu Kristo, amina.