Rafiki
Ahadi ya Ubatizo
Mei 2024


“Ahadi ya Ubatizo,” Rafiki, Mei 2024, 8–9.

Ahadi ya Ubatizo

“Kwa nini unataka kubatizwa?” Baba aliuliza.

Hadithi hii ilitokea huko Marekani.

“Baba, ninaweza kubatizwa wakati nitakapokuwa na umri wa miaka minane?” Keaton aliuliza.

Baba alitazama kutoka kwa mchezo waliokuwa wanacheza. “Huu ni uchaguzi mkubwa. Si ingekuwa bora kusubiri mpaka unapofika miaka 18?

Keaton alifikiria kuhusu hilo. “Lakini mimi nimekaribia miaka nane sasa. Na miaka 18 ni mbali sana!”

Baba alikuwa kimya kwa muda. Aliendelea kucheza mchezo. “Kwa nini unataka kubatizwa?”

“Ninampenda Yesu,” Keaton alisema. “Ninataka kumfuata Yeye.”

Hiyo ni sababu nzuri sana ya kubatizwa,” Baba alisema. Alitabasamu. “Nitakusaidia kama hicho ndicho unachochangua. Iwe una miaka minane au 18.”

Keaton alimkumbatia baba yake. “Asante!”

Baba hakuwa muumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Lakini bado alienda Kanisani pamoja na Keaton na Mama wakati mwingine. Na wakati Keaton alipotoa hotuba au kuimba pamoja na watoto wengine wa Msingi katika mkutano wa sakramenti, Baba daima alikuja.

Baada ya mchezo kwisha, Keaton alimpata Mama jikoni.

“Baba alisema ninaweza kubatizwa wakati nitakapokuwa na miaka minane,” alisema.

Mama alitabasamu. “Hiyo inapendeza sana! Je, ushafikiria kuhusu nani ungependa akubatize?”

Keaton anaweka sahani kwenye meza. “Unafikiri Babu anaweza?” Babu na Bibi walikuwa wanatumikia misheni katika jiji lingine.

“Tunaweza kuuliza,” Mama alisema.

Baada ya chakula cha jioni, Keaton alimpigia Babu na Bibi simu ya video kwenye simu ya Mama. Baada ya simu kuita kwa muda mchache, nyuso zao za tabasamu zilijaza skrini.

“Halo, Bibi! Halo, Babu!” Keaton alisema. Je, unajua kitu? Mimi nitabatizwa siku yangu ya kuzaliwa mwaka huu.”

“Hiyo inapendeza sana!” Bibi alisema.

“Babu, utanibatiza?” Keaton aliuliza.

Tabasamu la Babu likawa kubwa sana. “Ningependa iwe hivyo!”

Wakati siku yake ya kubatizwa ilipofika, Keaton alikuwa tayari. Mama na Baba walimwendesha kwa gari hadi kwenye kanisa dogo ambapo Bibi na Babu walikuwa wanatumikia misheni yao.

Keaton na Babu walivalia mavazi meupe. Walikaa pamoja wakati kila mmoja akiimba. Kisha Mama alisali.

Kisha, Baba akatoa hotuba. “Unapobatiwa, unaahidi kumfuata Yesu Kristo na kushika amri Zake. Yeye alitufundisha sisi kupendana. Upendo ndiyo njia bora ya kuishi,” yeye alisema.

Keaton aliitazama picha ya Yesu ambayo Baba alikuwa anashikilia.

“Tunapowapenda wengine, huwafanya wao kuhisi kwamba tunawajali. Pia hutusaidia kuwa na furaha na kuwa na amani. Baba alimtazama Keaton. “Nina shukrani kwamba wewe leo umeahidi kumfuata Yesu Kristo. Mimi ninatumaini ubatizo wako daima unakukumbusa wewe kumpenda Mungu na kuwapenda wengine.”

Keaton, alimpa Baba kumbatio kubwa. Kisha alimfuata Babu kwenye kisima kidogo. Keaton anaweka mkono mmoja kwenye mkono wa Babu na mwingine unashika mkono wa Babu. Babu alisema maneno ya sala ya ubatizo. Kisha alisaidia kumteremsha Keaton ndani ya maji.

Wakati Keaton alipotoka majini, alitabasamu. Ameweza! Amemfuata Yesu Kristo. Punde, pia angethibitishwa na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu. Kisha angekuwa muumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa siku za Mwisho.

Keaton alikuwa na hamu ya kushika ahadi yake ya kumkumbuka Yesu na kushika amri Zake.

Picha
Mwanamume mkongwe akimbatiza mvulana
Picha
PDF ya hadithi

Vielelezo na Alyssa Tallent

Chapisha