Rafiki
Shughuli za Njoo, Unifuate
Mei 2024


“Shughuli za Njoo, Unifuate,” Rafiki, Mei 2024, 28-29.

Njoo, Unifuate Shughuli za

Kwa ajili ya jioni ya nyumbani au kujifunza maandiko—au kwa ajili ya burudani tu!

Tembea katika Nyayo Zake

Mtoto akichora kufuatisha mguu

Kwa ajili ya Mosia 4–6

Mfalme Mosia alishika amri na “alitembea katika njia za Bwana” (Mosia 6:6). Kwenye kipande cha karatasi, chora kufuatisha mguu wako na kata umbo hilo. Andika kwenye mchoro wa mguu wako jinsi unavyoweza kumfuata Yesu. Weka mchoro wa mguu wako mahali ambapo unaweza kufuata mfano wa Yesu Kristo.

Mfuate Nabii

Msichana akichora kwenye dawati

Kwa ajili ya Mosia 7–10

Amoni alifundisha kwamba manabii wanaweza kuona vitu vitakavyokuja (ona Mosia 8:16–17). Nenda kwenye ukurasa wa 2 ili usome ujumbe wa Rais Nelson kutoka kwenye mkutano mkuu. Alitufundisha nini? Chora picha kuhusu jambo hilo alilofundisha na ututumie kwenye Rafiki.

Nuru Gizani

Watoto Wakiwa na kurunzi

Kwa ajili ya Mosia 11–17

Abinadi alifundisha kwamba Yesu Kristo ndiye “nuru isiyo na mwisho, ambayo haiwezi kutiwa giza” (Mosia 16:9). Ficha chombo katika nyumba. Zima taa na uache kila mtu ajaribu kukipata gizani. Kisha ficha chombo na mjaribu kukipata kama taa zimewashwa au kwa kutumia kurunzi. Ni njia gani ilikuwa rahisi? Je, ni kwa jinsi gani Yesu hutusaidia kama vile nuru ilivyokusaidia?

Mioyo Inafumwa katika Umoja

Watoto wamebeba mioyo ya karatasi

Kwa ajili ya Mosia 18–24.

Alma alitufundisha kuwa na “mioyo yetu kuunganishwa pamoja katika umoja na upendo” (Mosia 18:21). Hiyo inamaanisha tunapaswa kufanya kazi pamoja na kuonyesha upendo kwa wengine. Tengeneza mlolongo wa mioyo ili kukukumbusha! Kata kiasi cha mioyo ya karatasi na uandike jina la mwanafamilia katika kila moja. Toboa tundu katikati ya kila moyo na ipitishie uzi ili mioyo iwe imeunganika. Ning’iniza uzi wako wa mioyo mahali utakapoweza kuuona kila mara!

PDF ya hadithi

Vielelezo na Katy Dockrill