“Msafi Tena,” Rafiki, Mei 2024, 18–19.
Msafi Tena
Nisingeweza hata kuchagua kilicho sahihi hata kwa siku moja! Emily alifikiria.
Hadithi hii ilitokea huko Marekani.
Emily alisimama ndani ya maji pamoja na Baba na akatabasamu. Alikuwa amesubiria siku hii kwa wiki nyingi! Moyo wake ulikuwa unadunda kwa sababu yeye kamwe alikuwa hajawahi kuwa chini ya maji hapo awali. Lakini alikuwa na shauku kubwa ya kubatizwa kama Yesu Kristo alivyofanya.
Alifumba macho na kusikiliza Baba akisema sala ya ubatizo. Kisha aliziba pua yake, na kufumba macho, akakuja magoti yake Baba alipokuwa anamzamisha ndani ya maji.
Baba upesi alimtoa, na maji yakamtiririka. Emily alifuta macho yake, lakini alikuwa anatabasamu. Alihisi tofauti sasa. Hisia mpya, ya furaha ilimjaa. Alitaka kubaki na hisia hiyo daima!
Baba alimpa kumbatio kubwa. Ninajua jinsi ya kubakiza hisia hii nzuri, Emily alifikiria. Yote ninayohitaji ni kuchagua kilicho sahihi na kuwa kama Yesu Kristo! Alihisi kuwa hakika angeweza kufanya hivyo.
Walipofika nyumbani, Emily alikimbia kutoka garini hadi mlango wa mbele. Vivyo hivyo kaka yake wa miaka minne, Jonah. Wakati tu Emily alipofika mlangoni na kuanza kuufungua, Jonah alishika sketi yake na kuivuruta nyuma—kwa nguvu.
“Usithubutu!” Emily alifoka. Anavuta sketi yake kutoka mikononi yake. Kisha akamzibia njia ili asiwe wa kwanza kuingia ndani. Alijihisi kukasirika sana!
Ghafla akashtuka. Hisia mbaya zilimjaa. Akaondoka njiani na kumwacha Jonah kukimbia ndani.
“Pole!” alimwambia. Alikuwa amefanya uchaguzi mbaya. Mwokozi hangetaka yeye amfokee Jonah. Angekuwa ameharibu mambo kiasi gani? Hisia zake mpya zilikuwa zimeondoka.
Nimeharibu, yeye alifikiria. Nisingeweza hata kuchagua kilicho sahihi hata kwa siku moja!
Siku iliyofuata ilikuwa Jumapili. Emily alipokuwa tayari kwa ajili ya kwenda kanisa, alifikiria jinsi alivyomfokea Jonah. Bado alihisi vibaya.
Wakati wa mkutano wa sakramenti, askofu alimuomba Emily kuja mbele. Alikuwa athibitishwe. Hiyo ilimaanisha yeye angepata kipawa cha Roho Mtakatifu. Akaketi chini kwenye kiti. Baba pole pole aliweka mikono yake juu ya kichwa chake.
Emily alifumba macho yake wakati Baba alipoanza. Alimsikia yeye akisema maneno, “Pokea Roho Mtakatifu.”
Emily aliendelea kusikiliza.
“Emily, daima kumbuka kwamba kwa sababu ya Yesu Kristo, unaweza kutubu unapofanya uchaguzi usio sahihi,” Baba alisema. “Kila wakati unapopokea sakramenti, unaweza kufikiria agano ulilofanya ulipobatizwa. Unaweza kuahidi tena kumfuata Yeye.”
Baba alipomaliza baraka hiyo, Emily alihisi furaha na amani. Alijua Roho Mtakatifu alikuwa akiniambia kila kitu kingekuwa sawa. Ilikuwa SAWA kwamba yeye hakuwa mkamilifu. Kwa sababu ya Yesu Kristo na Upatanisho Wake, yeye angeweza kutubu na kusamehewa! Alisikitika kuwa alimfokea Jonah, na Baba wa Mbinguni alijua angeendelea kujaribu.
Emily alitabasamu wakati yeye na Baba walipokuwa wanaenda kwenye viti vyao. Sakramenti ndiyo ilifuata, na Emily anaitazamia sana.