“Mfalme Benyamini ni Nani?” Rafiki, Mei 2024, 24–25
Jifunze kuhusu Kitabu cha Mormoni
Mfalme Benyamini ni Nani?
Mfalme Benyamini alikuwa nabii wa Mungu na mfalme mwema. Aliwakusanya watu ili awafundishe. Alisimama mnarani ili watu wengi waweze kumsikia. Watu walipiga mahema kuzunguka mnara ili kusikiliza. Ilikuwa kama mkutano mkuu!
Mfalme Benyamini aliwafundisha kwamba Yesu Kristo angezaliwa duniani. Yesu angetenda miujiza. Angeteseka na kufa kwa ajili ya dhambi za watu wote. Angekufa pia na kufufuka ili tuweze kuishi tena!
Mfalme Benyamini aliwaalika watu kujichukulia juu yao jina la Kristo. Hiyo ilimaanisha wafanye agano, au ahadi, kumfuata Mungu na kushika amri Zake.
Leo, tunaonyesha kwamba tuko radhi kujichukulia juu yetu jina la Kristo wakati tunapobatizwa.
Changamoto ya Maandiko
-
Baada ya watu kumsikiliza Mfalme Benyamini, ni nani ambaye walifanya agano naye? (Mosia 5:5)
-
Ni kitu gani Abinadi alimwambia Mfalme Nuhu alihitaji kufanya ili kuokolewa? (Mosia 12:33)
-
Baada ya Alma na Helamu kutoka majini, walijawa na nini? (Mosia 18:14)
Ninaweza Kusoma Kitabu cha Mormoni!
Baada ya kusoma, paka rangi sehemu ya picha. Unaweza kusoma maandiko haya yanayoenda sambamba na usomaji wa kila wiki kutoka Njoo, Unifuate.
-
Wiki ya 1: Mosia 4:9
-
Wiki ya 2: Mosia 7:19
-
Wiki ya 3: Mosia 16:9
-
Wiki ya 4: Mosia 18:8–10