Rafiki
Kumfuata Yesu huko Vanuatu
Mei 2024


“Kumfuta Yesu huko Vanuatu,” Rafiki, Mei. 2024, 10-11.

Kumfuata Yesu huko Vanuatu

Kutana na Emma!

Jinsi Emma Anavyomfuata Yesu

Picha
Emma na dada yake chini ya mwamvuli

Emma anamfuata Yesu Kristo kwa kuwa mkarimu. Anataka kuwa rafiki wa wote! Anapenda kuzungumza na watu na kucheza michezo na watoto wengine. “Mimi ninapenda kucheza na marafiki zangu na kuwapa zawadi kwa sababu nawapenda watu,” Emma anasema. Wakati mwingine anatengeneza kadi kwa ajili ya marafiki na familia.

Emma pia humsaidia mama yake kuwatunza kaka zake wachanga ambao ni mapacha. Yeye husaidia kupika vyakula kwa ajili ya familia yao na kuwalisha kaka zake wachanga kwa chupa zao. “Ninahisi vizuri na furaha ninaposaidia. Ninajua kwamba Baba wa Mbinguni atanibariki,” Emma anasema.

Picha
Emma na famila yake

Kuhusu Emma

Picha
Picha ya Emma

Umri: miaka 10

Kutoka: Shefa, Vanuatu

Lugha: Kingereza, Kibislama, Kifiji,

Malengo: 1) Kwenda misheni. 2) Kuwa rubani

Michezo: Kuogelea na karaoke

Familia: Emma, Mama, Baba, dada mmoja na kaka wawili.

Mambo Ayapendayo Emma

Hadithi ya Kitabu cha Mormoni: Lehi na familia yake wakiondoka Yerusalemu (ona 1 Nefi 2)

Desturi ya likizo: Kugawa peremende na kadi kwa marafiki kwa ajili ya Pasaka

Matunda na mbogamboga: Ndizi, matufaa, machungwa, tikiti maji, letusi, karoti

Rangi: Waridi

Wimbo wa Msingi:“Families Can Be Together Forever,”(Kitabu cha Nyimbo za Watoto,188).

Picha
PDF ya hadithi

Chapisha