Rafiki
Ubatizo na Uthibitisho Ni Nini?
Mei 2024


“Ubatizo na Uthibitisho Ni Nini?” Rafiki, Mei 2024, 46–47

Misingi ya Injili

Ubatizo na Uthibitisho Ni Nini?

Picha
Msichana akibatizwa

Vielelezo na Apryl Stott

Yesu Kristo alibatizwa Baada kufika miaka minane, unaweza kubatizwa pia!

Wakati unapobatizwa, mwili wako wote unaingia ndani ya maji. Hii hutukumbusha sisi kwamba dhambi na chaguzi mbaya zinaweza kuoshwa kwa sababu ya Yesu Kristo.

Unamhaidi Baba wa Mbinguni kwamba utafanya kadiri uwezavyo kutii amri Zake.

Picha
Msichana akipokea baraka ya uthibitisho

Baada ya ubatizo huja uthibitisho. Hapo ndipo unapata kipawa cha Roho Mtakatifu. Hiyo humaanisha Roho Mtakatifu anaweza daima kuwa nawe! Anaweza kukusaidia kufuata mfano wa Yesu.

Chapisha