Rafiki
Nini kipo Akilini Mwako?
Mei 2024


“Nini kipo Akilini Mwako?” Rafiki, Mei 2024, 38.

Nini kipo Akilini Mwako?

Ni kwa jinsi gani nitajua kama ni Roho Mtakatifu au ni mimi?

—Prompted huko Paris

Mpendwa Prompted,

Roho Mtakatifu anaweza kukuongoza zaidi ya vile unavyofikiria. Kama umebatizwa na kuthibitishwa na unaendelea kufanya vyema uwezavyo kushika amri, wewe “daima Roho Wake atakuwa pamoja [nawe]” (Mafundisho na Maagano 20:77). Lakini unaweza kujuaje?

Roho Mtakatifu hutongoza sisi “kuwa wema” (Mafundisho na Maagano 11:12) na hutusaidia sisi “kujua ukweli wa mambo yote” (Moroni 10:5). Kama una wazo la kufanya kitu fulani kizuri au hisia ya upendo kwa ajili ya Mwokozi labda hiyo ni kutoka kwa Roho Mtakatifu!

Wakati mwingi, Roho Mtakatifu hatumii sauti kubwa au kukupa hisia kubwa kweli. Ni utulivu na amani. Kujifunza kumfuata Roho Mtakatifu kunaweza kuhitaji zoezi.

Unaweza kufanya hili!

Rafiki

Mawazo na hisia kutoka kwa Roho Mtakatifu huangaza njia yetu ya kurudi kwa Baba wa Mbinguni. Paka rangi kila balbu ya taa unaposoma baadhi ya njia ambazo Roho Mtakatifu anaweza kukusaidia.

Roho Mtakatifu anaweza . . .

  • kunijaza na upendo, furaha, amani, imani na tumaini.

  • kunipa mawazo ya kusaidia na kutumikia.

  • kunisaidia kukumbuka vitu vizuri.

  • kunisaidia kujua kile kilicho cha kweli.

  • kunisaidia kuelewa kile ninachojifunza.

Picha
PDF ya hadithi

Chapisha