Rafiki
Kushiriki Upendo wa Mungu
Mei 2024


“Kushirki Upendo wa Mungu,” Rafiki, Mei 2023, 32–33.

Kushiriki Upendo wa Mungu

Thais hakujua cha kusema au cha kufanya, lakini alitaka kusaidia.

Hadithi hii ilitokea huko Bolivia.

Ilikuwa asubuhi ya joto. Thais na rafiki yake Claudia walizungumza na kucheka walipokuwa wanatembea kuvuka uwanda wa mpira wa miguu. Walikuwa tu ndiyo wamemaliza darasa la mazoezi, na sasa walikuwa wanaenda kufanya hisabati.

Watoto wadogo walikuwa kwenye mapumziko. Thais aliwatazama wao wakicheza.

Kisha alimwona msichana mdogo akiwa peke yake kwenye ngazi. Walipofika karibu, Thais alimwona akilia.

Picha
Msichana mdogo akilia kwenye ngazi.

Thais alimpungia mkono Claudia kuja karibu na msichana mdogo.

Claudia alinuna na kutikisa kichwa kusema hapana, “Tutachelewa.”

Kabla ya Thais kusema chochote, Claudia alienda zake.

Thais alimtazama msichana mdogo. Alionekana kama ana miaka mitano. Uso wake ukiwa umefichwa katikati ya magoti yake, na akafunika kichwa chake na mikono yake.

Thais aliketi karibu naye. Msichana alisogea mbali kidogo.

Picha
Msichana mkubwa ameweka mkono juu ya bega la msichana mdogo

“Je, uko SAWA?” Thais aliuliza kwa upole.

Msichana hakujibu. Thais hakuwa na uhakika wa nini cha kusema au kufanya.

“Je, ninaweza kukusaidia? Kisha aliuliza.

Msichana aliinua mabega.

“Jina langu ni Thais. Jina lako ni nani?”

Mwishowe msichana alimtazama Thais. “Nicol.”

Kwa nini unalia, Nicol?”

“Kila mtu ananifanyia mzaha kwamba mimi ni kibonge,” alisema huku akilia.

Thais alimfuta Nicol uso. “Pole kwa wao kusema hivyo. Haijalishi kile watu wanafikiria.”

“Wanasema mimi si mrembo.”

“Sawa, nafikiria wao wamekosea!” Thais alisema kwa tabasamu. “Wewe ni mrembo na pia wewe ni maalumu sana. Je, ulijua hilo?

Thais alifikiria mojawapo ya nyimbo anazopenda kutoka Msingi. Alijua cha kusema sasa.

“Wewe ni mtoto wa Mungu, Thais alisema, akishikilia mikono ya msichana huyu.

Picha
Msichana mkubwa akishikilia mikono ya msichana mdogo

Thais alizungumza kidogo na Nicol. Alimwelezea jinsi Nicol alivyo muhimu kwa Baba wa Mbinguni, familia yake na wengine wengi ambao walimpenda yeye sana. Kidogo kidogo, Nicol alitabasamu.

Baada ya dakika chache, Nicol alisimama na kumkubatia Thais kwa nguvu. “Asante!” alisema.

Thais alimtazama rafiki yake mpya akikimbia akiwa na tabasamu kubwa. Alihisi vizuri kumsaidia Nicol kuhisi vyema na kujua jinsi Mungu anavyompenda yeye.

Kisha Thais akasimama pia. Ni vyema nikimbie kama Nicol la sivyo nitachelewa hisabati! alifikiria, akitabasamu alipokuwa akiharakisha kwenda darasani.

Picha
Msichana mdogo akikimbia akiwa na furaha
Picha
PDF ya hadithi

Vielelezo na Flavio Remontti

Chapisha