“Kutana na Mzee Patrick Kearon,” Rafiki, Mei 2024, 7.
Mtume Mpya Ameitwa
Kutana na Mzee Patrick Kearon
Imechukuliwa kutoka kwa Trent Toone, “uzoefu ‘mzuri’ wa maisha na ‘wenye kuhitaji mengi’ uliomwandaa Mzee Kearon kuwa Mtume,” Church News, Jan. 23, 2024.
Mzee Patrick Kearon ni mshiriki mpya wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili! Alizaliwa na kulelewa Uingereza. Yeye pamoja familia yake pia waliishi Saudi Arabia ambapo baba yake alikuwa na kazi huko. Aliitwa kama Mtume mnamo Desemba 7, 2023.
Akiwa kijana mkubwa, Mzee Kearon alikutana na wamisionari kutoka Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho huko London lakini hakuvutiwa na ujumbe wao. Baadae, wamisionari walianza kumfundisha kuhusu injili na aliguswa na Roho Mtakatifu. Wakati alipokuwa akijifunza zaidi juu ya kanisa, Mzee Kearon alipokea baraka za ukuhani. Alisema lilikuwa tukio zuri ambalo lilimsaidia kufanya uamuzi wa kujiunga na Kanisa. Alibatizwa siku ya mkesha wa Krismas alipokuwa na umri wa miaka 26.
Mzee Kearon na mkewe, Jennifer, wana watoto wanne. Mtoto wao wa kwanza alifariki angali mchanga. Huu ulikuwa ni muda wa huzuni kubwa kwa Mzee na Dada Kearon. Lakini ilisaidia kuimarisha imani yao katika ufufuko na injili ya Yesu Kristo. Mzee Kearon aliitwa kama Kiongozi Mkuu Mwenye Mamlaka wa Sabini mwaka 2010 . Anapenda kuona waumini wa Kanisa wakiwasaidia watu wenye shida ulimwenguni kote.
Mzee Kearon anashukuru kwa mpango wa wokovu. Anafahamu kwamba hata wakati wa kipindi kigumu tunaweza siku zote kuuhisi upendo wa Baba wa Mbinguni na Mwokozi.