Ibada na Maagano Ni Nini? Rafiki, Mei 2024, 22.
Kadi za Mahekalu
Ibada na Maagano Ni Nini?
Ibada ni tendo takatifu linalofanywa kwa mamlaka ya ukuhani, kama vile ubatizo na sakramenti. Agano ni ahadi tunayofanya na Baba wa Mbinguni kupitia ibada za ukuhani. Ibada na maagano hutusaidia kukua karibu zaidi na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Siku moja unaweza kufanya maagano zaidi hekaluni.
Hekalu la Port Vila Vanuatu
-
Hili litakuwa hekalu la kwanza huko Vanuatu.
-
Litakuwa kwenye kisiwa cha Efate, mojawapo ya karibia visiwa 80 katika nchi hiyo.
-
Hekalu lililo karibu ni zaidi ya maili 700 (Kilomita 1,127) huko Fiji.
Hekalu la Neiafu Tonga
-
Hili litakuwa hekalu la pili huko Tonga.
-
Wamisionari wa kwanza walikuja Tonga mnamo 1891. Sasa kuna waumini wengi huko.
-
Mfalme na malkia wa Tonga walikuwepo wakati wa ufunguzi wa kuchimbua msingi wa ujenzi wa hekalu.