Rafiki
Watu wa Alma Wanasali Mioyoni Mwao
Mei 2024


“Watu wa Alma Wanasali Mioyoni Mwao,” Rafiki, Mei 2024, 26–27.

Hadithi za Maandiko

Watu wa Alma Wanasali Mioyoni Mwao

Picha
Alma akiwafundisha watu

Vielelezo na Andrew Bosley

Picha
Alma akimbatiza mtu fulani

Alma alikuwa nabii aliyewafundisha watu. Wale walioamini walibatizwa. Walifanya agano kumfuata Mungu.

Picha
Amuloni akimkaripia mfanyakazi mwenza

Mtu mwovu aliyeitwa Amuloni alikuwa mtawala wa watu wa Alma. Alikuwa mkatili sana kwao. Aliwafanya wao wabebe mizigo mizito.

Picha
Watu wakisali

Alma na watu wake walisali kwa ajili ya msaada. Lakini Amuloni aliweka sheria kwamba mtu yeyote ambaye angepatikana akisali angeuawa.

Watu waliacha kusali kwa sauti. Lakini waliendelea kusali mioyoni mwao. Mungu alijibu sala zao.

Picha
Watu wakifanya kazi kwa mwonekano wa amani.

Mungu alijua walikuwa wamefanya agano Naye. Aliahidi kuwafanya wao wawe na nguvu. Aliwafariji na kuifanya mizigo yao kuwa miepesi. Baadaye, Mungu hata aliwasaidia wao kumtoroka Amuloni na kusafiri hadi mahali salama.

Chapisha