Rafiki
Muda wa Hadithi za Maandiko
Mei 2024


“Muda wa Hadithi za Maandiko,” Rafiki, Mei 2024, 30–31.

Muda wa Hadithi za Maandiko

“Je, kuna mtu yeyote aliye na kitabu anataka nikisome leo?” Bw. Otoo aliuliza.

Hadithi hii ilitokea huko Ghana.

“Huu ni wakati wa kusoma,” Bw, Otoo alisema.

Nyameye aliketi wima. Muda wa kusoma ni burudani!

Kila siku shuleni, mwalimu wao alisoma kitabu kwa sauti darasani. Wakati mwingine alisoma kuhusu wanyama. Wakati mwingine alisoma kuhusu watu katika nchi zingine. Na wakati mwingine aliuliza darasa kama walikuwa na kitabu wangetaka yeye asome.

“Je, kuna mtu yeyote aliye na kitabu anataka nikisome leo?” Bw. Otoo aliuliza.

Nyameye alinyanyua mkono wake. “‘Ninacho!’” Alitwaa mkoba wake na kutoa kitabu chake anachokipenda. Ilikuwa ni kitabu cha hadithi za Kitabu cha Mormoni! Alikileta ili kukisoma baada ya shule wakati akimsubiri mama yake kumchukua. Kuona picha hizi kulimsaidia kuelewa hadithi za maandiko.

Bw. Otoo alitabasamu wakati alipoona kitabu kikubwa. “Hatutakuwa na muda wa kukisoma chote. Je, kuna sehemu fulani ungependa mimi nisome?”

“Ndiyo,” Nyameye alisema. Alifungua kurasa mpaka akapata hadithi yake anayoipenda. “Je, unaweza kusoma hii, tafadhali? Inaitwa Ndoto ya Lehi.”

“Je, hii hadithi ni kuhusu nini? Bw. Otoo aliuliza.

“Kuhusu nabii ambaye aliona ono. Aliona mti mzuri ulio na tunda tamu.” Nyameye alionyesha picha ya mti. “Alitaka familia yake pia wale tunda lile pamoja naye. Je, utasoma?” Nyameye akampa mwalimu wake kitabu hicho.

“Bila shaka,” Bw. Otoo alisema. Kisha alianza kusoma kwa sauti. Alisoma kuhusu njia nyembamba inayoelekeza kwenye mti. Alisoma kuhusu fimbo ya chuma. Na alisoma kuhusu kushika amri.

Picha
Mwalimu akiwasomea watoto kitabu

Selorm rafiki ya Nyameye alinyanyua mkono wake. “Ulikuwa mti wa aina gani?” Alimuuliza Nyameye.

“Sijui,” Nyameye alisema. “Lakini tunda lilikuwa zuri sana. Lazima likuwa hata bora kuliko mti wa maembe!” Kisha Nyameye aliacha kufikiria. “Kanisani, nilijifunza kwamba tunda huwakilisha upendo wa Mungu. Ndiyo maana lilikuwa tamu sana na maalumu!”

Wakati darasa lilipomalizika, Nyameye alikaa nje kumsubiri mama yake. Alitoa kitabu chake cha Kitabu cha Mormoni ili kusoma zaidi.

“Hiyo ilikuwa ni hadithi nzuri,” Selorm alisema. Aliketi karibu na Nyameye. “Je, naweza kusoma nyingine pamoja nawe?”

“Ndiyo!” Nyameye alifungua hadithi nyingine. Walisoma kuhusu Abinadi na Mfalme Nuhu.

Wengi wa wanadarasa wao walikuja kusikiliza. Wakati walipokuwa na maswali, Nyameye aliwajibu. Hata aliwauliza wao maswali ili kuwahoji kuhusu hadithi walizosoma!

Punde Nyameye alimwona mama yake akitembea kuwaelekea. “Asante kwa kusoma pamoja nami,” aliwaambia watoto wengine. Alifunga kitabu na kutabasamu. Alifurahia kwamba marafiki zake walipenda hadithi zake kama vile yeye alivyozipenda.

Picha
PDF ya hadithi

Vielelezo na Zhen Liu

Chapisha