“Mazungumzo na Isabela kuhusu Maagano,” Rafiki, Jan. 2024, 40–41.
Mazungumzo na Isabela kuhusu Maagano
Isabela anatokea Alajuela, Costa Rica. Tulimuuliza yeye baadhi ya maswali kuhusu kile inachomaanisha kushika maagano yake ya ubatizo.
Tuambie kuhusu wewe mwenyewe.
Nina umri wa miaka 13. Ninapenda kucheza mpira wa miguu, kupika, kushona, kuogelea na kuwatumikia wengine. Ndoto yangu likuwa ni kuwa daktari wa wanyama kwa sababu ninapenda kuwasaidia wanyama. Chakula changu pendwa ni piza na tambi na rangi yangu pendwa ni zambarau.
Ni kwa jinsi gani unayashika maagano yako ya ubatizo?
Ninatubu na kupokea sakramenti kila wiki. Nina wito katika darasa langu la Wasichana, na ninajaribu kufanya kwa bidiii. Pia ninashika maagano yangu kwa kuwatumikia wengine.
Je, unafanya nini ili kuwatumikia wengine?
Ninapenda kuisaidia familia yangu. Kila mara ninacheza na binamu yangu wa miaka mitatu, Lina, wakati wazazi wake wanafanya kazi. Ninapenda kumsaidia Babu yangu na Bibi yangu wanaponihitaji. Pia ninamsaidia mwanadarasa wangu kujifunza kwa ajili ya mtihani wake wa Kifaransa shuleni.
Niambie zaidi kuhusu wito wako!
Mimi ni mshauri wa kwanza katika darasa langu la Wasichana. Wajibu wangu unajumuisha kuwahudumia wasichana. Hii humaanisha kuwasiadia wao na chochote wanachohitaji. Ninaenda darasani na kwenye shughuli, na ninajaribu kuwa rafiki wa wasichana wengine katika darasa langu ambao hawaji kanisani.
Ni ushauri upi ungempa mtu kuhusu wito wake wa kwanza?
Ningependa kuwaambia kwamba hawahitaji kuwa na uoga. Wito ni njia tu unayoweza kusaidia katika kazi ya Baba wa Mbinguni. Njia nzuri zaidi kuweza kuwasaidia wengine ni kupitia mfano wako!