Rafiki
Muhtasari wa Mkutano
Mei 2024


“Muhtasari wa Mkutano,” Rafiki, Mei 2024, 5.

Muhtasari wa Mkutano

Ahadi za Maagano

Dallin H. Oaks

Rais Oaks alifundisha kwamba agano ni ahadi ya kufanya mambo fulani. Kwa mfano, madaktari na zima moto wanafanya agano la kuwasaidia watu katika jumuia zao. Tunapofanya maagano na Baba yetu wa mbinguni, kama vile tunapobatizwa, tunaahidi kumtumikia Yeye na kuzitii amri Zake. Yeye anatubariki sisi tunaposhika maagano yetu.

Hii inanifundisha mimi:

Kofia ya zima moto na stetoskopu.

Endelea kupiga makasia.

Dale G. Renlund

Mzee Renlund alisimulia kuhusu safari kwa kutumia mtumbwi wa Kieskimo ambapo alipiga kasia mbele zaidi ya familia yake. Aliposimama, wimbi lilimwangusha ndani ya maji. Mwongozaji alimwambia aendelee kupiga kasia ili asonge mbele na asianguke. Kama tukiendelea “kupiga kasia” kuelekea kwa Mwokozi, tunaweza kuwa salama na kulindwa.

Hii inanifundisha:

Mtumbwi na mpiga kasia

Kupata Ushuhuda

Mark L. Pace

Rais Pace alishiriki jinsi gani wakati alipokuwa na umri wa miaka 11, mama yake alimuuliza kama yeye binafsi alifahamu kwamba injili ni ya kweli. Aliamua kusoma Kitabu cha Mormoni na kusali ili apate kujua. Kadiri alivyofanya, alijisikia faraja na amani kutoka kwa Roho Mtakatifu. Hii ilimsaidia yeye kupata ushuhuda wake mwenyewe.

Hii inanifundisha mimi:

Fungua kitabu

Mawe matano

Andrea Muñoz Spannaus

Dada Spannaus alisimulia hadithi ya Daudi na Goliathi. Kama vile Daudi alivyokuwa na mawe matano ili kupigana na Goliathi, yapo mawe “matano” ya kukusaidia wewe ukabiliane na changamoto katika maisha. Haya ni upendo kwa Mungu, imani katika Yesu Kristo, kujua kwamba wewe ni mwana wa Mungu, toba ya kila siku, na ufikiaji kwenye nguvu ya Mungu.

Hii inanifundisha:

Kombeo na mawe
Ukurasa wa PDF

Vielelezo na Josh Talbot