Rafiki
Kumsikiliza Roho Mtakatifu
Mei 2024


“Kumsikiliza Roho Mtakatifu,” Rafiki, Mei 2024, 39.

Imeandikwa na Wewe

Kumsikiliza Roho Mtakatifu

Picha
Mvulana akifanya umbo la kikombe ili kusikia

Siku moja wakati wa jioni ya nyumbani, mama yangu alikuwa anazungumza kuhusu Roho Mtakatifu. Alisema kwamba mara nyingi Roho Mtakatifu husema kwa kukupa wazo ndani ya akili yako.

Wakati aliposema hilo, nilishangaa sana. Mapema tu siku hiyo, nilikuwa nimesali na kumwomba Baba wa Mbinguni anisaidie kumsikia Roho Mtakatifu. Lakini sikujua kwamba Roho Mtakatifu angeweza kusema nami ndani ya akili yangu jinsi hiyo. Maisha yangu yote nimekuwa na mawazo ambayo yaliniongoza kuchagua jema. Sasa nilijua kwamba mawazo haya yalitoka kwa Roho Mtakatifu!

Tangu wakati huo, nimemtambua Roho Mtakatifu zaidi. Jumapili iliyopita tu, tulikuwa tuna jioni ya nyumbani tena. Wakati huu ilikuwa kuhusu ushuhuda. Kwa kweli sikujua ushuhuda ilikuwa ni nini, kwa hiyo nilimuuliza baba yangu. Aliniambia kwamba ushuhuda ni kitu unachojua au kuamini ni cha kweli. Alisema tunapata shuhuda zetu kutoka kwa Roho Mtakatifu. Kisha nikafikiria jinsi nilivyoanza kumtambua Roho Mtakatifu zaidi, na BOOM! Mimi pia nilikuwa na ushuhuda!

Kujua hili hunifanya nihisi kuwa na furaha sana. Ninataka kuwa mfuasi mwema wa Yesu Kristo na daima kumsikiliza Roho Mtakatifu.

Picha
PDF ya hadithi

Vielelezo na Brenna Vaughan

Chapisha