Rafiki
Ukarimu Wakati wa Chakula cha Mchana
Mei 2024


“Ukarimu Wakati wa Chakula cha Mchana,” Rafiki, Mei 2024, 36–37.

Ukarimu Wakati wa Chakula cha Mchana

Je, wavulana wengine wakubwa wangemfanyia mzaha pia?

Hadithi hii ilitokea huko Ufilipino.

Dave alimsikia mama yake akibisha mlango wa chumba chake cha kulala. Ulikuwa muda wa kuamka. Aliondoka kitandani na kunawa uso wake. Kisha akaungana na Mama, Baba na ndugu zake kwenye chumba cha mbele.

“Habari ya asubuhi,” Mama alisema. Dave alitabasamu kwa usingizi. Familia ilipiga magoti, na Baba alitoa sala ya kuanza siku yao.

“Ninataka kushiriki maandiko mazuri asubuhi hii,” Mama alisema. Alifungua Kitabu cha Mormoni. “Hii ni Moroni 7:45. ‘Na hisani huvumilia, na ni karimu,’”

Dave alifikiria kuhusu maandiko haya alipokuwa akiwa tayari kwenda shule. Kabla ya kuondoka mlangoni, alitoa sala. “Tafadhali nisaidie kuwa mkarimu leo.” alisali.

Darasani, Dave alihisi furaha alipokuwa anafanya kazi yake ya shuleni. Alisikiliza kwa makini Mwalimu Frida alipowapa baadhi ya maneno mapya ya tahajia ya kujifunza.

Punde ulifika muda wa chakula cha mchana. Dave alikuwa amebeba viazi vitamu na juisi baridi. Aliketi chini pamoja na marafiki zake na wakaanza kuzungumza.

Punde alisikia baadhi ya watoto kwenye meza iliyo karibu. Wavulana wawili walikuwa wanamfanyia mzaha mvulana mpya aliyeitwa Jose. Jose alikuwa mdogo kwa umri wake, lakini alikuwa mpole kwa wengine na alifanya bidii darasani. Wavulana wengine walikuwa na chakula cha mchana, lakini Jose hakuwa nacho.

“Kwa nini wewe ni mdogo hivi? “Je, hamna chakula nyumbani?” Antonio aliuliza.

Dave aligeuka kuwaangalia wavulana wale na kumwona Joaquin akichukua mkoba wa Jose na kumtupia Antonio. Jose alimkimbiza Antonio ili kupata vitu vyake.

“Tafadhali nipe mkoba wangu,” Jose alisema.

Picha
Dave akitazama nyuma huku wavulana wakitwaa mkoba wa Jose

Lakini Antonio na Joaquin hawakusikia. “Mkoba wako umezeeka sana na ni mbaya!” Joaquin alisema.

Dave alisikia maneno yote ya kuhudhi, lakini alikuwa mwoga kumsaidia Jose. Je, wale watoto wengine wangefikiria vipi? Je, Joaquin na Antonio wangemfanyia mzaha pia?

Kisha alifikiria kuhusu maandiko ambayo Mama alisoma asubuhi. Hisani ni ukarimu. Yesu Kristo angemtaka yeye kuwa mkarimu. Ilikuwa ni kitu sahihi cha kufanya.

Dave alijikakamua na kuwakabili wavulana wengine. “Acheni kumfanyia mzaha Jose. Tafadhali mpeni mkoba wake.

“Je, tatizo lako ni nini? Joaquin aliuliza.

“Kwa nini nyinyi ni wakatili hivyo kwa Jose? Hakufanya kosa lolote,” Dave alisema. Kisha alivuta pumzi ndefu. “Yesu anatupenda sisi sote, na Yeye anataka sisi tuwe wakarimu. Tafadhalini acheni kumfanyia mzaha Jose. Uonevu ni makosa. Kama mtaendelea kufanya hivyo, nitamwita Mwalimu Frida.”

Antonio alitazama viatu vyake. Alimpa Jose mkoba wake. “Pole,” alimunyamunya. Yeye na Joaquin walirudi kwenye viti vyao.

“Asante,” Jose alisema.

Dave alimgusa Jose begani. “Sasa sisi ni marafiki.”

Jose alitabasamu.

Nyumbani, Dave aliiambia familia yake kile kilichotokea.

“Hiyo haikuwa rahisi, lakini ulifanya kitu sahihi.” Baba alisema.

“Mimi ninajivunia kwa kuwa ulikuwa mkarimu,” Mama alisema.

Siku iliyofuata Mama alipokuwa akimsaidia kuweka chakula chake cha mchana, Dave aliuliza, “Tafadhali tunaweza kutengeneza sandwichi mbili?”

“Kwa nini?” “Je, una njaa kiasi hicho?” Mama aliuliza.

Dave alicheka. “Hapana, lakini jana niliona Jose hakuwa na chakula. Nataka kugawa chakula changu.”

“Hilo ni wazo zuri sana!” Mama akatoa mkate zaidi na Dave akatengeneza sandwichi nyingine.

Wakati wa chakula cha mchana, Dave na Jose waliketi na kula sandwichi zao pamoja. Ilibidi kuwa jasiri kuwazuia watoto wengine kumuonea Jose. Lakini Dave alimpenda rafiki yake mpya, na alijua Baba wa Mbinguni alifurahia kwamba yeye alichagua kuwa mkarimu.

Picha
Dave na Jose wanakula pamoja
Picha
PDF ya hadithi

Vielelezo na Mark Robison

Chapisha