Rafiki
Wapendwa Wazazi
Mei 2024


“Wapendwa wazazi,” Rafiki, Mei. 2024, jalada la nyuma.

Wapendwa Wazazi,

Sakramenti ni zawadi kutoka kwa Mwokozi ya kutusaidia sisi kumkumbuka na kumfuata Yeye kila wiki. Mnaweza kusoma “Msafi Tena” (ukurasa wa 18) ili kuwasaidia watoto wenu wakubwa kufikiria kuhusu jinsi sakramenti hutusaidia kushika maagano yetu. Pamoja na watoto wadogo, someni “Ninaweza Kumfuata Yesu kwa Kupokea Sakramenti” (ukurasa wa 44). Zungumzeni kuhusu kile tunachofanya wakati wa kila sehemu ya sakramenti. Mngeweza pia kusoma sala za sakramenti pamoja na watoto wenu. Waache wanyanyue juu picha ya Yesu kila wakati wanaposikia jina Lake. Hii itawasaidia wao kumfikiria Yeye wakati wa sakramenti.

Kwa Upendo,

Rafiki

Picha
Ukurasa wa PDF

Chapisha