“Salamu kutoka Vanuatu!” Rafiki, Mei 2024, 12–13
Salamu kutoka Vanuatu!
Jifunze kuhusu watoto wa Baba wa Mbinguni ulimwenguni kote.
Vanuatu ni nchi ya kisiwa cha kitropiki huko Bahari ya Pasifiki. Zaidi ya watu elfu mia tatu wanaishi huko!
Lugha
Kibislama, Kingereza na Kifaransa ndiyo lugha rasmi. Karibu kila mtu anaongea Kibislama!
Kitabu cha Mormoni
Kitabu cha Mormoni kilitafsiriwa kwa Kibislama mwaka 2004. Tangu wakati huo, karibia zaidi ya watu 8,000 wamejiunga na Kanisa huko Vanuatu!
Kisiwa cha Tropiki
Vanuatu inajulikana kwa pwani zake maridadi na maji safi ya buluu. Baadhi ya pwani hata zina changarawe nyeusi!
Fedha maridadi
Vanuatu ina fedha za rangi angavu ambazo zinaonyesha mandhari kutoka kwenye maisha ya kisiwani na miti na wanyama wanaoishi hapo.