Rafiki
Nguvu ya Hekalu
Mei 2024


“Nguvu ya Hekalu,” Rafiki, Mei 2024, 2–3.

Ujumbe wa Mkutano kutoka kwa Nabii

Nguvu ya Hekalu

Imechukuliwa kutoka kwenye “Furahia katika Zawadi ya Funguo za Ukuhani,” Liahona, Mei 2024, 119–21.

Mnamo Machi, Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho lilinunua Hekalu la Kirtland. Hekalu hili lilikuwa sehemu muhimu ya urejesho wa injili ya Yesu Kristo.

Mnamo Aprili 3, 1836 Yesu Kristo aliwatokea Joseph Smith na Oliver Cowdery ndani ya Hekalu hili la Kirtland. Mwokozi alilikubali hekalu hili kama nyumba Yake. Yeye kisha akaahidi, “Nami nitajionesha kwa watu wangu kwa rehema katika nyumba hii” (Mafundisho na Maagano 110:7). Ahadi hii inatumika kwa kila hekalu leo hii.

Ndani ya hekalu, unaweza kupokea majibu ya sala. Unaweza pia kupokea imani, uwezo, faraja, maarifa, na nguvu. Muda katika hekalu utakusaidia kufikiria selestia na kuona wewe ni nani hasa na unaweza kuwa nani. Utakusaidia uelewe ni kwa jinsi gani wewe unafaa vizuri katika mpango mkuu wa Mungu. Ninakuahidi hilo.

Hekalu la Kirtland

Hekalu la Kirtland

Shughuli-ya-Kukata

Kata kuzunguka kingo za Hekalu la Kirtland. Kisha Kunja kwenye mistari ya nukta na fungamanisha pembe na dari pamoja.

Hekalu la Kirtland ni Nini?

Hekalu la Kirtland lilijengwa huko Kirtland, Ohio, Marekani, mwaka 1836. Lilikuwa hekalu la kwanza la Kanisa lililorejeshwa.

Baadae, waumini wa Kanisa walitakiwa kuliacha na kwenda magharibi. Kanisa lingine lilitunza jengo hilo kwa miaka mingi. Hivi karibuni, Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho limelinunua hekalu hili.

Ukurasa wa PDF

Michoro na David Green