Ndani ya Kina cha Mioyo Yetu
Bwana anajaribu kutusaidia—sisi sote—kupata injili Yake ndani ya kina cha mioyo yetu.
Akina dada na akina kaka, tunaishi katika wakati wa kupendeza sana hivi sasa. Tunaposherehekea mwanzo wa Urejesho, inafaa pia kusherehekea Urejesho unaoendelea ambao tunaushuhudia. Ninafurahia pamoja na wewe kuishi katika siku hii.1 Bwana anaendelea kuweka yote pamoja, kupitia manabii Wake, yote ambayo yanahitajika kutusaidia kujiandaa kumpokea Yeye.2
Mojawapo ya vitu hivyo vinavyohitajika ni mpango mpya wa Watoto na Vijana. Wengi wenu mnajua mkazo wa programu hii kwenye kuweka malengo, nembo mpya za kuwa sehemu ya, na mikutano ya Kwa Nguvu ya Vijana. Lakini hatupaswi kuruhusu hayo yazibe mtazamo wetu juu ya kanuni ambazo kwazo programu hii imejengwa na malengo yake: kusaidia kupata injili ya Yesu Kristo ndani ya kina cha mioyo ya watoto na vijana wetu.3
Ninaamini tunapofahamu kanuni hizi kwa uwazi zaidi, tutaona hii kama zaidi ya programu ya washiriki wa miaka 8 hadi 18. Tutaona jinsi Bwana anavyojaribu kutusaidia—sisi sote—kupata injili Yake kwa kina ndani ya mioyo yetu. Ninaomba Roho Mtakatifu atusaidie kujifunza pamoja.
Mahusiano—“Kuwa pamoja Nao”4
Kanuni ya kwanza ni mahusiano. Kwa sababu wao ni sehemu ya asili ya Kanisa la Yesu Kristo, wakati mwingine tunasahau umuhimu wa mahusiano katika safari yetu endelevu kwa Kristo. Hatutegemewi kupata au kutembea njia ya agano peke yake. Tunahitaji upendo na msaada kutoka kwa wazazi, wanafamilia wengine, marafiki, na viongozi ambao pia wako kwenye njia.
Aina hizi za mahusiano huchukua muda. Muda wa kuwa pamoja. Muda wa kucheka, kucheza, kujifunza na kutumikia pamoja. Muda wa kuthamini masilahi na changamoto za kila mmoja. Muda wa kuwa wawazi na waaminifu kwa kila mmoja pale tunapojitahidi kuwa bora pamoja. Mahusiano haya ni moja ya malengo ya kukusanyika kama familia, akidi, madarasa, na mikutano. Haya ni msingi wa huduma madhubuti.5
Mzee Dale G. Renlund alitupa ufunguo wa kukuza mahusiano haya wakati aliposema: “Ili kuwatumikia wengine vizuri lazima tuwaone … kupitia macho ya Baba wa Mbingu. Ni hapo tu ndipo tunaweza kuelewa thamani halisi ya nafsi. Ni hapo tu ndipo tunaweza kuhisi upendo alionao Baba wa Mbinguni kwa watoto Wake wote.”6
Kuwaona wenzetu kama vile Mungu anavyowaona ni kipawa. Ninawaalika kila mmoja wetu kutafuta kipawa hiki. Wakati macho yetu yamefunguliwa kuona,7 tutaweza pia kuwasaidia wengine kujiona kama Mungu anavyowaona.8 Rais Henry B. Eyring alisisitiza nguvu ya hili wakati aliposema: “Kilicho muhimu zaidi ni nini [wengine] wanachojifunza kutoka [kwako] juu ya wao ni nani hasa na kile hasa wanachoweza kuwa. Nadhani kwamba hawatajifunza mengi kuhusu hilo kutoka kwenye mihadhara. Watakipata kutokana na hisia za wewe ni nani, unadhani wao ni akina nani, na kile unachodhani wanaweza kuwa.”9 Kuwasaidia wengine kuelewa utambulisho wao wa kweli na lengo lao halisi ni moja ya zawadi kubwa tunazoweza kutoa.10 Kuwaona wengine na sisi wenyewe vile Mungu anavyotuona huunganisha mioyo yetu “kwa pamoja katika umoja na katika upendo.”11
Kwa nguvu za ulimwengu zinazoongezeka kila wakati kutuvuta, tunahitaji nguvu inayotokana na mahusiano ya upendo. Kwa hivyo tunapopanga shughuli, mikutano, na mikusanyiko mingine, hebu tukumbuke kusudi kuu la mikusanyiko hii ni kujenga mahusiano ambayo hutuimarisha na kusaidia kupata injili ya Yesu Kristo ndani ya kina cha mioyo yetu.12
Ufunuo, Haki ya kujiamulia, na Toba—“Waunganishe na Mbingu”13
Kwa kweli, haitoshi tu kufungwa pamoja. Kuna vikundi na mashirika mengi ambayo yanafikia umoja kupitia sababu tofauti. Walakini umoja tunaotafuta ni kuwa wamoja katika Kristo, kujiunganisha sisi pamoja na Yeye.14 Ili kuunganisha mioyo yetu na mbingu, tunahitaji uzoefu binafsi wa kiroho, kama vile Mzee Andersen alivyotoka kutuzungumzia hilo kwa ushawishi.15 Uzoefu huo huja wakati Roho Mtakatifu anapopeleka neno na upendo wa Mungu kwenye akili na mioyo yetu.16
Ufunuo huu unakuja kupitia maandiko, hasa Kitabu cha Mormoni; kupitia maneno yenye msukumo wa Kiungu kutoka kwa manabii walio hai na wafuasi wengine waaminifu; na kupitia sauti ndogo, tulivu.17 Maneno haya ni zaidi ya wino kwenye ukurasa, mawimbi ya sauti kwenye masikio yetu, mawazo katika akili zetu, au hisia katika mioyo yetu. Neno la Mungu ni nguvu ya kiroho.18 Ni ukweli na nuru.19 Ni jinsi tunavyomsikia! Neno linaanzisha na kuongeza imani yetu kwa Kristo na linachochea ndani yetu hamu ya kuwa kama Mwokozi—ambayo ni, kutubu na kutembea njia ya agano.20
Aprili mwaka jana, Rais Russell M. Nelson alitusaidia kuelewa jukumu kuu la toba katika safari hii iliyofunuliwa.21 Alisema: “Tunapochagua kutubu, tunachagua kubadilika! Tunamruhusu Mwokozi kutubadilisha kuwa toleo bora zaidi la sisi wenyewe. … Tunachagua kuwa zaidi kama Yesu Kristo!”22 Mchakato huu wa badiliko, unaochochewa na neno la Mungu, ndivyo jinsi tunavyoungana na mbingu.
Msingi wa mwaliko wa Rais Nelson wa kutubu ni kanuni ya haki ya kujiamulia. Tunapaswa kuchagua toba sisi wenyewe. Injili haiwezi kulazimishwa kuingia kwenye mioyo yetu. Kama Mzee Renlund alivyosema, “Lengo la Baba yetu wa Mbinguni katika malezi sio kuwafanya watoto Wake wafanye yaliyo sahihi; ni kufanya watoto wake wachague kufanya yaliyo sahihi.”23
Katika programu iliyobadilishwa na watoto na Vijana, kulikuwa na mahitaji tofauti zaidi ya 500 ya kukamilisha ili kupokea utambulisho mbali mbali.24 Leo, kimsingi kuna moja. Ni mwaliko wa kuchagua kuwa zaidi kama Mwokozi. Tunafanya hivi kwa kupokea neno la Mungu kupitia Roho Mtakatifu na kumruhusu Kristo atubadilishe kuwa “toleo bora zaidi la sisi wenyewe.”
Hii ni zaidi ya mazoezi ya kuweka malengo au kujiboresha. Malengo ni nyenzo tu ambayo hutusaidia kuungana na mbingu kupitia ufunuo, haki ya kujiamulia, na toba—kuja kwa Kristo na kupokea injili yake kwa kina ndani ya mioyo yetu.23
Ushiriki na Dhabihu—“Waruhusu Wao Waongoze”25
Mwishowe, ili kupata injili ya Yesu Kristo ndani ya kina cha mioyo yetu, tunahitaji kujihusisha nayo—kutoa muda wetu na talanta zetu kwa ajili yake, kutoa dhabihu kwa ajili yake.26 Sote tunataka kuishi maisha ya maana, na hii ni kweli hasa kwa kizazi kinachoinukia. Wanatamani kusudi.
Injili ya Yesu Kristo ndilo kusudi kuu zaidi ulimwenguni. Rais Ezra Taft Benson alisema: “Tumeamriwa na Mungu kuchukua injili hii kwa ulimwengu wote. Hilo ndilo kusudi ambalo lazima lituunganishe leo. Injili tu ndiyo itaokoa ulimwengu kutokana na janga la kujiangamiza wenyewe. Injili tu ndiyo itawaunganisha wanaume [na wanawake] wa kila kabila na mataifa kwa amani. Injili tu ndiyo italeta furaha, shangwe na wokovu kwa familia ya binadamu.”27
Mzee David A. Bednar aliahidi, “Tunapowawezesha vijana kwa kuwaalika na kuwaruhusu kuchukua hatua, Kanisa litasonga mbele kwa njia za kimiujiza.”28 Mara nyingi hatujawaalika na kuwaruhusu vijana kujitolea kwa kusudi hili kuu la Kristo. Mzee Neal A. Maxwell alisema, “Ikiwa vijana [wetu] wamelemewa na [kazi ya Mungu], wana uwezekano mkubwa wa kulemewa na ulimwengu.”29
Programu ya Watoto na Vijana inafokasi kwenye kuwawezesha vijana. Wanachagua malengo yao wenyewe. Urais wa akidi na madarsa huwekwa katika majukumu yao sahihi. Baraza la vijana la kata, kama vile baraza la kata, linafokasi kwenye kazi ya wokovu na kuinuliwa.30 Na akidi na madarasa huanza mikutano yao kwa kushauriana juu ya jinsi ya kufanya kazi ambayo Mungu amewapa.31
Rais Nelson aliwaambia vijana wa Kanisa: “Ukichagua, ikiwa unataka, … unaweza kuwa sehemu kubwa ya kitu kikubwa, kitu kizuri, kitu adhimu! … Wewe ni miongoni mwa bora zaidi ambao Bwana amewahi kuwaleta kwenye ulimwengu huu. Una uwezo wa kuwa nadhifu na mwenye busara na una athari zaidi juu ya ulimwengu kuliko kizazi chochote kilichopita!”32 Katika hafla nyingine, Rais Nelson aliwaambia vijana: “Nina ujasiri kamili kwenu. Ninawapenda na Bwana pia anawapenda. Sisi ni watu Wake, tuliojiunga pamoja katika kazi Yake takatifu.”33 Vijana, je! Mnaweza kuhisi imani ambayo Rais Nelson anayo kwenu na jinsi gani mlivyo muhimu katika kazi hii?
Wazazi na viongozi watu wazima, ninawaombeni muwaone vijana kama Rais Nelson anavyowaona. Wakati vijana wanapohisi upendo wako na imani yako, unapowahimiza na kuwafundisha jinsi ya kuongoza—na kisha kutoka kwenye njia yao—watakushangaza kwa ufahamu wao, uwezo wao, na kujitolea kwao kwenye injili.34 Watasikia furaha ya kuchagua kujihusisha na kujitolea kwa ajili ya kusudi la Kristo. Injili Yake itaingia ndani ya kina cha mioyo yao, na kazi itasonga mbele kwa njia za kimiujiza.
Ahadi na Ushuhuda
Ninaahidi, tunapofokasi kwenye kanuni hizi—mahusiano, ufunuo, haki ya kujiamulia, toba, na dhabihu—injili ya Yesu Kristo itazama ndani ya kina cha mioyo yetu sote. Tutaona Urejesho ukisonga mbele hadi kwenye kusudi lake la mwisho, ukombozi wa Israeli na kuanzishwa kwa Sayuni,35 ambapo Kristo atatawala kama Mfalme wa wafalme.
Ninashuhudia kwamba Mungu anaendelea kufanya vitu vyote muhimu kuandaa watu wake kwa ajili ya siku hiyo. Na tuuone mkono wake katika kazi hii tukufu pale sote tunapojitahidi “kuja kwa Kristo, na kufanywa kamili ndani yake.”36 Katika Jina la Yesu Kristo, amina.