Mkutano Mkuu
Shangwe za Hosana
Mkutano mkuu wa Aprili 2020


Shangwe za Hosana

Sasa, kaka na dada zangu wapendwa, tunapokumbuka Ono la Kwanza la Joseph smith la Baba na Mwana, tumeona kwamba itakuwa vyema kufurahi pamoja kwa kushiriki katika Shangwe za Hosana.

Shangwe hizi takatifu zilitolewa kwa mara ya kwanza katika kipindi hiki cha maongozi ya Mungu katika uwekaji wakfu Hekalu la Kirtland mnamo Machi 27, 1836. Na sasa zinatolewa kwenye uwekaji wakfu wa kila hekalu. Ni shukrani takatifu kwa Baba na Mwana, zikiashiria hisia za umati wakati Mwokozi alipoingia Yerusalemu kwa ushindi. Pia zinatoa uthibitisho wa kile Joseph mdogo alichopitia siku ile katika Msitu Mtakatifu—kinachojulikana, kwamba Baba na Mwana ni Viumbe wawili waliotukuka ambao tunawaabudu na kuwasifu.

Sasa nitaonesha jinsi Shangwe za Hosana zinavyotolewa. Ninapofanya hivyo, ninawaalika wenzetu wa vyombo vya habari kulichukulia adhimisho hili takatifu kwa hadhi ya utu na heshima.

Kila anayeshiriki huchukua leso safi nyeupe, akiishikilia katika kona mojawapo, na kuipunga wakati tukisema kwa pamoja, “Hosana, Hosana, Hosana kwa Mungu na Mwanakondoo,” ikirudiwa mara tatu, kisha ikifuatiwa na “Amina, Amina, na Amina.” Kama huna leso nyeupe, unaweza kupunga tu mkono wako.

Akina kaka na akina dada, sasa ninawaalika kusimama na kushiriki katika Shangwe za Hosana, baada ya hili “Wimbo wa Hosana” na “Roho wa Mungu”1 zitaimbwa.

Kufuatia ishara kutoka kwa mwongozaji, tafadhali jiunge katika kuimba “Roho wa Mungu.”

Hosana, Hosana, Hosana kwa Mungu na Mwanakondoo.

Hosana, Hosana, Hosana kwa Mungu na Mwanakondoo.

Hosana, Hosana, Hosana kwa Mungu na Mwanakondoo.

Amina, Amina, na Amina.

Muhtasari

  1. Nyimbo za Kanisa, na. 2.

Chapisha