Mkutano Mkuu
Kuidhinisha Viongozi Wakuu wenye Mamlaka, Sabini wa Maeneo, na Maafisa Wakuu
Mkutano mkuu wa Aprili 2020


Kuidhinisha Viongozi Wakuu wenye Mamlaka, Sabini wa Maeneo, na Maafisa Wakuu

Akina kaka na akina dada, sasa nitawasilisha kwenu Viongozi Wakuu Wenye Mamlaka, Sabini wa Maeneo, na Maafisa Wakuu wa Kanisa kwa ajili ya kura yenu ya kuwakubali.

Tafadhali onesha kura yako katika njia iliyozoeleka popote ulipo. Kama kuna wale waliopinga mapendekezo yoyote yaliyowasilishwa, tunaomba kwamba muwasiliane na rais wenu wa kigingi.

Inapendekezwa kwamba tumkubali Russell Marion Nelson kama nabii, mwonaji, na mfunuzi na Rais wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho; Dallin Harris Oaks kama Mshauri wa Kwanza katika Urais wa Kwanza; na Henry Bennion Eyring kama Mshauri wa Pili katika Urais wa Kwanza.

Wale wanaounga mkono, waoneshe.

Wale wanaopinga, kama wapo, wanaweza kuonesha.

Inapendekezwa kwamba tumkubali Dallin H. Oaks kama Rais wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili na M. Russell Ballard kama Kaimu Rais wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili.

Wale wanaounga mkono, tafadhali onesheni.

Yeyote anayepinga anaweza kuonesha.

Inapendekezwa kwamba tuwakubali wafuatao kama washiriki wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili: M. Russell Ballard, Jeffrey R. Holland, Dieter F. Uchtdorf, David A. Bednar, Quentin L. Cook, D. Todd Christofferson, Neil L. Andersen, Ronald A. Rasband, Gary E. Stevenson, Dale G. Renlund, Gerrit W. Gong, na Ulisses Soares.

Wale wanaounga mkono, tafadhali dhihirisheni.

Yeyote anayepinga anaweza kuonyesha.

Inapendekezwa kwamba tuwakubali washauri katika Urais wa Kwanza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili kama manabii, waonaji, na wafunuzi.

Wote wanaounga mkono, tafadhali onesheni.

Kinyume, kama kuna yeyote, kwa ishara hiyo hiyo.

Inapendekezwa kwamba tuwapumzishe wafuatao kama Sabini wa Maeneo: Mzee Jorge T. Becerra, Mark S. Bryce, Jeremy R. Jaggi, Kelly R. Johnson, Adeyinka A. Ojediran, na Moisés Villanueva.

Wale wanaopenda kuungana pamoja nasi katika kutoa shukrani kwa huduma yao nzuri, tafadhali wadhihirishe.

Inapendekezwa kwamba tuwapumzishe kwa moyo wa shukrani Urais Mkuu wa Wavulana kama ifuatavyo: Stephen W. Owen kama Rais, Douglas D. Holmes kama Mshauri wa Kwanza, na M. Joseph Brough kama Mshauri wa Pili.

Wale wote wanaopenda kuungana nasi katika kutoa shukrani kwa akina kaka hawa kwa huduma yao ya kusifika, tafadhali waoneshe.

Inapendekezwa kwamba tuwakubali wafuatao kama Sabini Wakuu Wenye Mamlaka: Jorge T. Becerra, Matthew S. Holland, William K. Jackson, Jeremy R. Jaggi, Kelly R. Johnson, Thierry K. Mutombo, Adeyinka A. Ojediran, Ciro Schmeil, na Moisés Villanueva.

Wote wanaounga mkono, tafadhali onesheni.

Wale wanaopinga, kwa ishara hiyo hiyo.

Inapendekezwa kwamba tuwakubali wafuatao kama Sabini wa Maeneo: Jay D. Andersen, Faapito Auapaau, Frederick K. Balli Jr., Kevin W. Birch, John W. Boswell III, J. Francisco Bührer, Suchat Chaichana, Matthew R. Clarke, L. Guido Cristobal, Edmarc R. Dumas, Carlos A. Gabaldón, M. Andrew Galt IV, Clark G. Gilbert, Leonard D. Greer, Vladislav Y. Gornostaev, D. Martin Goury, Richard I. Heaton, Broc C. Hiatt, David H. Huntsman, Norman C. Insong, Daniel Kabason, Federico M. Kähnlein, Jeffrey J. Kerr, Youngjoon Kwon, David G. LaFrance, Ricardo C. Leite, Marcelo Louza, Jose G. Manarin, Jeremiah J. Morgan, Mark A. Mortensen, Eduardo F. Ortega, Nathan D. Pace, Michael M. Packer, Omar I. Palacios, Jorge W. Pérez, Kyrylo Pokhylko, Sergio A. Poncio, Arthur Rascon, Miguel A. Reynoso, Gustavo G. Rezende, Robert G. Rivarola, Tonga J. Sai, Luciano Sankari, Rosendo Santos, Henry Savstrom, J. Matthew Scott, James E. Slaughter, Robert T. Smith, Ricardo A. Spencer, Colin C. Stauffer, David C. Stewart, Jared W. Stone, Arlen M. Tumaliuan, Martin J. Turvey, Yan C. Vega, Paul B. Whippy, Chad R. Wilkinson, na Dow R. Wilson.

Wote wanaounga mkono, tafadhali onesheni.

Wale wanaopinga, ikiwa kuna yeyote.

Inapendekezwa kwamba tuwakubali kama Urais Mkuu mpya wa Wavulana Steven J. Lund kama Rais, Ahmad Saleem Corbitt kama Mshauri wa Kwanza, na Bradley Ray Wilcox kama Mshauri wa Pili.

Wale wanaounga mkono, waoneshe.

Yeyote anayepinga anaweza kuonesha vivyo hivyo.

Inapendekezwa kwamba tuwakubali Viongozi wengine Wakuu Wenye Mamlaka, Sabini wa Maeneo, na Maafisa wakuu kama ilivyo sasa.

Wote wanaounga mkono, tafadhali onesheni.

Wale wanaopinga, ikiwa kuna yeyote.

Kwa mara nyingine, tunawaalika wale ambao inawezekana wamepinga mapendekezo yoyote kuwasiliana na marais wao wa vigingi.

Tunawashukuru kwa imani yenu endelevu na sala kwa niaba ya viongozi wa Kanisa.

Chapisha