Mkutano Mkuu
Kuwakubali Viongozi Wakuu wenye Mamlaka, Sabini wa Maeneo, na Maafisa Wakuu
Mkutano mkuu wa Oktoba 2023


4:29

Kuwakubali Viongozi Wakuu wenye Mamlaka, Sabini wa Maeneo na Maafisa Wakuu

Akina kaka na akina dada, ni heshima kwangu kuwasilisha kwenu Viongozi Wakuu Wenye Mamlaka, Sabini wa Maeneo na Maafisa Wakuu wa Kanisa kwa ajili ya kura yenu ya kuwakubali.

Tafadhali onesha kukubali kwako katika njia iliyozoeleka, popote ulipo. Kama kuna wale waliopinga, tunaomba kwamba muwasiliane na rais wenu wa kigingi.

Inapendekezwa kwamba tumkubali Russell Marion Nelson kama nabii, mwonaji, na mfunuzi na Rais wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho; Dallin Harris Oaks kama Mshauri wa Kwanza katika Urais wa Kwanza; na Henry Bennion Eyring kama Mshauri wa Pili katika Urais wa Kwanza.

Wale wanaounga mkono, waoneshe.

Wale wanaopinga, kama wapo, wanaweza kuonesha.

Inapendekezwa kwamba tumkubali Dallin H. Oaks kama Rais wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili na M. Russell Ballard kama Kaimu Rais wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili.

Wale wanaounga mkono, tafadhali onesheni.

Yeyote anayepinga anaweza kuonesha.

Inapendekezwa kwamba tuwakubali wafuatao kama washiriki wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili: M. Russell Ballard, Jeffrey R. Holland, Dieter F. Uchtdorf, David A. Bednar, Quentin L. Cook, D. Todd Christofferson, Neil L. Andersen, Ronald A. Rasband, Gary E. Stevenson, Dale G. Renlund, Gerrit W. Gong, na Ulisses Soares.

Wale wanaounga mkono, tafadhali onyesheni.

Yeyote anayepinga anaweza kuonyesha.

Inapendekezwa kwamba tuwakubali washauri katika Urais wa Kwanza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili kama manabii, waonaji na wafunuzi.

Wote wanaounga mkono, tafadhali onesheni.

Kinyume, kama kuna yeyote, kwa ishara hiyo hiyo.

Kama ilivyotangazwa awali, tumetoa mwito kwa Lexander Dushku kutumikia kama Kiongozi Mkuu Mwenye Mamlaka wa Sabini.

Wale wanaounga mkono, tafadhali onyesheni.

Wale wanaopinga, kwa ishara hiyo hiyo.

Tunatambua pia kwa shukrani kupumzishwa kwa Sabini wa Maeneo wawili ambao majina yao yanaweza kupatikana katika tovuti ya Kanisa.

Wale wanaotaka kuungana pamoja nasi katika kuonyesha shukrani zetu kwa ndugu hawa kwa huduma yao bora wanaweza kuonyesha.

Inapendekezwa kwamba tuwakubali Viongozi Wakuu Wenye Mamlaka wengine, Sabini wa Eneo—ikijumuisha Sabini wa Eneo wawili wapya waliotangazwa mapema wiki hii ambao majina yao yameorodheshwa katika tovuti hii ya Kanisa, na Maafisa Wakuu kama ilivyo sasa.

Wote wanaounga mkono, tafadhali onesheni kwa kuinua mkono.

Wale wanaopinga, ikiwa kuna yeyote.

Tunawashukuru, akina kaka na akina dada, kwa imani na sala zenu endelevu kwa niaba ya viongozi wa Kanisa.

Mabadiliko kwa Sabini wa Eneo

Sabini wa Eneo wafuatao waliidhinishwa wakati wa kikao cha uongozi kilichofanyika kama sehemu ya mkutano mkuu:

Rogério Boschi na Kirt L. Hodges.

Sabini wa Eneo wafuatao walipumzishwa wakati wa kikao cha uongozi kilichofanyika kama sehemu ya mkutano mkuu:

Henry J. Eyring na Youngjoon Kwon.