Mkutano mkuu wa Oktoba 2023 Kikao cha Jumamosi Asubuhi Kikao cha Jumamosi Asubuhi David A. BednarKwenye Njia ya Jukumu LaoMzee Bednar anaelezea shukrani yake kwa waumini wa Kanisa ambao wanahudumu kote ulimwenguni na ni nguvu ya Kanisa. Amy A. WrightStahimili Siku katika KristoDada Wright anafundisha kwamba kupitia msaada wa Yesu Kristo, sote tunaweza “kustahimili siku” na kupambana na kushinda changamoto tunazokabiliana nazo. Robert M. DainesBwana, Tungependa Kumwona YesuMzee Daines anafundisha kanuni ili kutusaidia kumwona vyema Mwokozi na kuelewa upendo wa Mungu. Carlos A. GodoyKwa Manufaa ya Vizazi VyakoMzee Godoy anawataka wale ambao wamesonga mbali au si waaminifu kama wanavyotakiwa kuwa kurudi ili wao pamoja na uzao wao waweze kufurahia baraka za injili. D. Todd ChristoffersonNguvu ya KuunganishaMzee Christofferson anafundisha kwamba nguvu ya kuunganisha ambayo huhalalisha ibada zote za ukuhani na kuzifanya zifungwe kote duniani na mbinguni, ni ya muhimu kwa ajili ya kukusanya Israeli. Ian S. ArdernMpende Jirani YakoMzee Ardern anafundisha kwamba juhudi za kibinadamu ni njia za kuonesha huruma kwa wengine na kufuata amri ya Bwana ya “mpende jirani yako.” Dallin H. OaksFalme za UtukufuRais Oaks anafundisha kuhusu falme za utukufu baada ya maisha haya na fokasi ya Kanisa katika kutusaidia kuhitimu kwa ajili ya daraja la juu la ufalme wa Selestia. Kikao cha Jumamosi Mchana Kikao cha Jumamosi Mchana Henry B. EyringKuwakubali Viongozi Wakuu wenye Mamlaka, Sabini wa Maeneo, na Maafisa WakuuRais Eyring anawasilisha Viongozi Wakuu Wenye Mamlaka, Sabini wa Maeneo, na Maafisa Wakuu kwa ajili ya kura ya kuwakubali. Neil L. AndersenZaka: Kufungua Madirisha ya MbinguniMzee Andersen anafundisha kwamba tunapolipa zaka kwa uaminifu, Bwana atafungua madirisha ya mbinguni na kumwaga baraka juu yetu. Jan E. NewmanKuhifadhi Sauti ya Watu wa Agano katika Kizazi KinachoinukiaKaka Newman anafundisha kwamba ni jukumu la wazazi kuwafundisha watoto wao kuja kwa Yesu Kristo. Joaquin E. CostaNguvu ya Yesu Kristo Katika Maisha Yetu Kila SikuMzee Costa anafundisha kwamba tunaweza kupata nguvu katika imani yetu katika katika Yesu Kristo tunapotafuta kuja Kwake na kila siku. Gary E. StevensonMinong’ono ya RohoMzee Stevenson anafundisha umuhimu wa kutafuta, kutambua, na kutenda juu ya minong’ono ya Roho Mtakatifu. Yoon Hwan ChoiJe, Unataka Kuwa na Furaha?Mzee Choi anafundisha kwamba kama tunataka kuwa na furaha, tunapaswa kubaki kwenye nyia ya agano. Bwana atatubariki na kubeba mizigo yetu. Alan T. PhillipsMungu Anakujua na AnakupendaMzee Phillips anafundisha kwamba sisi ni watoto wa Mungu, kwamba Yesu Kristo anatukomboa na kutuletea msaada, na kwamba Baba wa Mbinguni ni mkamilifu na mwenye upendo. Ronald A. RasbandItakuwa Shangwe Kubwa Namna Gani KwakoMzee Rasband anafundisha kwamba ili kukusanya Israeli, wamisionari wengi wanahitajika na anawaalika watu wazima wachukue maarifa na shuhuda zao na kwenda misheni. Kikao cha Jumamosi Jioni Kikao cha Jumamosi Jioni Gary B. SabinSifa Bainifu za FurahaMzee Sabin anafundisha njia tano za kupata furaha ya kweli. Joni L. KochMnyenyekevu Kukubali na KufuataMzee Koch anafundisha umuhimu wa kuwa mnyenyekevu na kutumaini katika Bwana. Tamara W. RuniaKuiona Familia ya Mungu kupitia Lenzi ya UjumuishiDada Runia anafundisha kwamba kuna nguvu na shangwe wakati tunapojiona sisi na familia zetu kutokea kwenye mtazamo wa picha kubwa. Ulisses SoaresAkina Kaka na Akina Dada katika KristoMzee Soares anafundisha jinsi ya kujilinda dhidi ya chuki na kutendeana kama akina kaka na akina dada katika Yesu Kristo. Kikao cha Jumapili Asubuhi Kikao cha Jumapili Asubuhi M. Russell BallardSifa kwa Aliyenena na BwanaRais Ballard anashuhudia juu ya baraka nyingi tunazozifurahia kwa sababu ya Nabii Joseph Smith, ambaye alirejesha utimilifu wa injili ya Yesu Kristo. Emily Belle FreemanKutembea katika Uhusiano wa Agano na KristoRais Freeman analinganisha kutembea njia ya agano na kutembea Njia ya Yesu huko Israeli. Adilson de Paula ParrellaKutoa Ushahidi juu ya Yesu Kristo kwa Maneno na MatendoMzee Parrella anafundisha kwamba tunaweza kujichukulia jina la Mwokozi juu yetu sisi kwa kutoa ushuhuda juu Yake kwa maneno na matendo yetu. Quentin L. CookKuweni Wafuasi wa Amani wa KristoMzee Cook anafundisha kwamba wafuasi wa amani wa Kristo ambao wanashika amri Zake watabarikiwa kwa amani wanapokabiliana na majaribu na wanaweza kutazamia siku zijazo angavu. Dieter F. UchtdorfMpotevu na Njia Ambayo Inaongoza NyumbaniMzee Uchtdorf anafundisha kwamba kamwe hakuna kuchelewa kwenye kutubu na kurejea kwenye njia iongozayo kwa Mungu. W. Christopher WaddellZaidi ya ShujaaAskofu Waddell anafundisha kwamba katika mashujaa wote, Yesu Kristo ni mkuu. Henry B. EyringMwenzi Wetu DaimaRais Eyring anafundisha kwamba tunahitaji kujitahidi kuwa na Roho Mtakatifu kama mwenzi wetu daima. Kikao cha Jumapili Mchana Kikao cha Jumapili Mchana Dale G. RenlundYesu Kristo ni HazinaMzee Renlund anafundisha kwamba tunapofokasi kwa Yesu Kristo na kuacha kutazama kupita alama, tutapata hazina kubwa ya injili. John C. Pingree Jr.Ukweli wa MileleMzee Pingree anafafanua ukweli ni nini, kwa nini ni muhimu, jinsi gani tunaweza kuupata na jinsi tunavyopaswa kuushiriki na wengine. Valeri V. CordónMasomo ya Uzazi wa KiunguMzee Cordón anafundisha kwamba wazazi wanapaswa kuwafundisha watoto wao utamaduni wa injili na kuwasaidia kuwaongoza warejee mbinguni. J. Kimo EsplinNguvu ya Uponyaji ya Mwokozi juu ya Visiwa vya BahariMzee Esplin anashiriki hadithi kuhusu Mtakatifu wa Siku za Mwisho Mjapani anayeonyesha nguvu ambayo tunaweza kuipata katika maagano ya hekaluni. Gerrit W. GongUpendo Unazungumzwa HapaMzee Gong anafundisha jinsi tunavyoweza kutumia lugha tatu za upendo wa injili: lugha ya uchangamfu na staha, lugha ya huduma na dhabihu na lugha ya kuwa sehemu ya agano. Christophe G. Giraud-CarrierSisi ni watoto WakeMzee Giraud-Carrier anafundisha kwamba lazima tukumbuke kwamba sote tu watoto wa Mungu na lazima tupendane, bila kujali tofauti zetu. Russell M. NelsonFikiria Selestia!Rais Nelson anafundisha umuhimu wa kuwa na imani katika Yesu Kristo na kufanya chaguzi ukifikiria ufalme wa selestia.