Mkutano Mkuu
Sifa Bainifu za Furaha
Mkutano mkuu wa Oktoba 2023


Sifa Bainifu za Furaha

Kujenga juu ya msingi wa Yesu Kristo ni muhimu kwa furaha yetu.

Nikiwa kwenye safari ya ndege ya kibiashara miaka kadhaa iliyopita, nilijikuta nimeketi karibu na mwanaume kutoka Uholanzi. Nilikuwa na hamu ya kuzungumza naye kwa kuwa nilitumikia Ubelgiji na Uholanzi nikiwa mmisionari kijana.

Tulipofahamiana, alinipa kadi yake ya biashara yenye jina la kipekee la kazi ya “profesa wa furaha.”  Nilitoa maoni juu ya taaluma yake ya kushangaza na nikamuuliza ni nini profesa wa furaha alifanya. Alisema aliwafundisha watu jinsi ya kuwa na maisha yenye furaha kwa kuanzisha Uhusiano na malengo yenye maana. Nilimjibu, “Hiyo ni nzuri sana, lakini vipi ikiwa ungeweza pia kufundisha jinsi Uhusiano huo unavyoweza kuendelea zaidi ya kaburi na kujibu maswali mengine ya nafsi, kama vile kusudi la maisha ni nini, tunawezaje kushinda udhaifu wetu na wapi tunaenda baada ya sisi kufa?” Alikiri kwamba ingependeza ikiwa tungekuwa na majibu ya maswali hayo, na nilifurahi kushiriki naye kwamba tunayo.

Leo, ningependa kupitia kanuni chache muhimu za furaha ya kweli ambazo zinaonekana kuepukwa na watu wengi katika ulimwengu huu wenye kutatanisha, ambapo mambo mengi yanapendeza lakini machache ni muhimu sana.

Alma aliwafundisha watu wa siku zake, “Kwani tazama, ninawaambia kuna vitu vingi vitakavyokuja; na tazama, kuna kitu kimoja ambacho ni muhimu kuliko vyote—kwani tazama, wakati hauko mbali ambao Mkombozi ataishi miongoni mwa watu wake.”1

Tamko hili ni muhimu vile vile kwetu leo tunapotazamia na kujitayarisha kwa Ujio wa Pili wa Kristo!

Kwa hivyo, uchunguzi wangu wa kwanza ni kwamba kujenga juu ya msingi wa Yesu Kristo ni muhimu kwa furaha yetu. Huu ni msingi thabiti, “msingi ambao watu wakijenga juu yake hawawezi kuanguka.”2 Kufanya hivyo hututayarisha kukabiliana na changamoto za maisha, kwa liwalo lo lote.

Miaka mingi iliyopita, nilienda kwenye kambi ya Skauti wakati wa kiangazi pamoja na mtoto wetu Justin. Shughuli zilipokuwa zikiendelea, alitangaza kwa furaha kwamba yeye na marafiki zake walitaka kupata beji ya sifa ya kurusha mishale. Kufanya hivyo kuliwahitaji wavulana kupita mtihani mfupi wa kuandika na kulenga shabaha kwa mishale yao.

Moyo wangu ulifadhaika. Wakati huo, Justin alikuwa dhaifu kabisa kutokana na ugonjwa wa kupooza misuli, ugonjwa ambao alikuwa akipambana nao tangu kuzaliwa. Nilijiuliza ikiwa angeweza kuvuta upinde nyuma kiasi cha kupeleka mshale kwenye shabaha.

Yeye na marafiki zake walipoondoka kuelekea darasa la wapiga mishale, nilisali kimya kimya kwamba asifedheheshwe na uzoefu huo. Saa kadhaa za wasiwasi baadaye, nilimwona akija kwangu akiwa na tabasamu kubwa. “Baba!” Alishangaa. “Nimepata beji ya kustahili! Nimelenga katikati; ilikuwa kwenye shabaha iliyo karibu nami, lakini nililenga shabaha sahihi!” Alikuwa ameuvuta upinde kwa nguvu zake zote na kuuacha ule mshale uruke, asiweza kudhibiti uelekeo wake. Ninashukuru sana kwa yule mwalimu mwelewa wa kurusha mishale, ambaye hakusema kamwe, “Pole, shabaha isiyofaa!” Badala yake, alipoona mapungufu na jitihada ya Justin, alijibu kwa wema, “Kazi nzuri!”

Hivyo ndivyo itakavyokuwa kwetu ikiwa tutajitahidi kadiri tuwezavyo kumfuata Kristo na manabii Wake licha ya mapungufu yetu. Ikiwa tunasonga Kwake kwa kushika maagano yetu na kutubu dhambi zetu, tutasikia kwa furaha pongezi za Mwokozi wetu: “Vema, wewe mtumishi mwema na mwaminifu.”3

Ninawatolea ninyi ushuhuda wangu juu ya uungu wa Mwokozi wa ulimwengu na wa upendo Wake wa ukombozi na uwezo wa kuponya, kuimarisha na kutuinua tunapojitahidi kwa dhati kujongea Kwake. Kinyume chake, haiwezekani kujongea pamoja na umati wa watu na pia kuelekea kwa Yesu. Mwokozi ameshinda kifo, magonjwa, na dhambi na ametoa njia ya ukamilifu wetu wa pekee ikiwa tutamfuata kwa mioyo yetu yote.4

Uchunguzi wangu wa pili ni kwamba ni muhimu kwa furaha yetu kwamba tukumbuke kwamba sisi ni wana na mabinti wa Baba wa Mbinguni mwenye upendo. Kujua na kuamini ukweli huu hubadilisha kila kitu.

Miaka kadhaa iliyopita, kwenye safari ya ndege kuelekea nyumbani kutoka kwenye kazi ya Kanisa, mimi na Dada Sabin tulijikuta tumeketi moja kwa moja nyuma ya mtu mkubwa sana ambaye alikuwa na uso mkubwa, wa hasira uliochorwa chale kwenye sehemu ya nyuma ya upara wake na kuandika nambari 439.

Tulipotua, nilisema, “Samahani, bwana. Kama hutojali naweza kuuliza umuhimu wa nambari iliyochorwa nyuma ya kichwa chako?” Sikuthubutu kuuliza uso ule wenye hasira.

Akasema, “Huyo ni mimi. Huyo ndiye mimi. Ninamiliki himaya hiyo: 219!”

Mia nne thelathini na tisa ndiyo ilikuwa nambari halisi kichwani mwake, kwa hiyo nilishangaa alipoikosea kwani ilikuwa muhimu sana kwake.

Nilifikiria jinsi gani ilivyohuzunisha kwamba utambulisho na heshima kwa mtu huyu kulitegemea nambari inayohusishwa na himaya ya genge la wahalifu. Nilijiwaza mwenyewe, mwanamume huyu mwenye sura ngumu wakati mmoja alikuwa mvulana mdogo ambaye bado alihitaji kuhisi kuwa wa thamani na kujumuishwa. Laiti angejua yeye alikuwa nani hasa na ni mali ya nani hasa, kwa maana sote “tumenunuliwa kwa bei.”5

Kuna mstari wa busara katika wimbo wa filamu The Prince of Egypt ambao unasema, “Angalia maisha yako kupitia macho ya mbinguni.”6 Ufahamu wa ukoo wetu wa kiungu na uwezekano wetu wa milele unapozama ndani ya nafsi zetu, tutaweza kuona maisha kama tukio lenye kusudi, linaloendelea kujifunua la kujifunza na kukua, hata kama “tunaona katika kioo, kwa jinsi ya fumbo”7 kwa msimu mfupi.

Sifa bainifu ya tatu ya furaha ni kukumbuka kila wakati thamani ya nafsi. Tunafanya hivi vyema zaidi kwa kufuata mawaidha ya Mwokozi “pendaneni; kama nilivyowapenda ninyi.”8

Pia alifundisha, “Kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.”9

Kitabu cha Mithali kinashauri kwa hekima: “Usiwanyime watu mema yaliyo haki yao, ikiwa katika uwezo wa mkono wako kuyatenda.”10

Hatutajuta kuwa wakarimu kupita kiasi. Machoni pa Mungu, ukarimu ni sawa na ukuu. Kama sehemu ya kuwa wakarimu ni kusamehe na kutohukumu.

Miaka mingi iliyopita, familia yetu changa ilikuwa ikienda kuangalia sinema kwa ajili ya jioni ya familia nyumbani. Sote tulikuwa ndani ya gari isipokuwa mmoja wa wana wetu na mke wangu, Valerie. Tayari giza lilikuwa limeingia, na mtoto wetu alipofungua mlango na kukimbilia kwenye gari, kwa bahati mbaya alipiga teke kwenye kibaraza kile alichodhani kuwa ni paka wetu. Bahati mbaya kwa mtoto wetu na mke wangu, ambaye alikuwa nyuma yake, hakuwa paka wetu badala yake kicheche asiye na furaha, ambaye aliwafundisha adabu! Sote tulirudi ndani, ambapo wote wawili walioga na kuosha nywele zao kwa juisi ya nyanya, dawa iliyodhaniwa ya uhakika ya kuondoa harufu ya kicheche huyo. Kufikia wakati walipokuwa wamejisafisha na kubadilisha nguo zao, sote tulikuwa hatuhisi harufu yo yote, kwa hivyo tuliamua kwamba tulikuwa sawa kwenda kwenye sinema. 

Mara tu tulipokaa nyuma ya ukumbi wa sinema, mmoja baada ya mwingine watu waliokuwa karibu nasi waliamua ghafla kwenda nje kuchukua bisi. Waliporudi, hata hivyo, hakuna aliyerudi kwenye kiti chake cha awali.

Tulicheka tunapokumbuka tukio hilo, lakini vipi ikiwa dhambi zetu zote zingekuwa na harufu? Ingekuwaje ikiwa tungeweza kunusa harufu ya ukosefu wa uaminifu, tamaa, wivu au kiburi? Udhaifu wetu wenyewe ukiwa umefunuliwa, tunatumaini kwamba tungekuwa wenye kufikiria na kuwa waangalifu zaidi kwa wengine na, vivyo hivyo wao kwetu, pale tunapofanya mabadiliko yanayohitajika katika maisha yetu. Ninapenda harufu ya tumbaku kanisani, kwa sababu inaonyesha mtu anajaribu kubadilika. Wanahitaji mikono yetu ya kuwakaribisha karibu nao.

Raisi Russell M. Nelson kwa hekima amesema, “Njia moja rahisi ya kumtambua mfuasi wa kweli wa Yesu Kristo ni kwa huruma kiasi gani mtu huyo huwatendea wengine.”11

Paulo aliwaandikia Waefeso, “Tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.”12

Kama wafuasi wa Yesu Kristo, tunaombwa kumtumaini Baba wa Mbinguni na Mwokozi wetu na tusijaribu kuweka mbadala Wao. Yesu Kristo anajua kutokamilika kwa kila mtu kikamilifu na atahukumu kikamilifu.

Sifa yangu bainifu ya nne ya furaha ni kudumisha mtazamo wa milele. Mpango wa Baba yetu unaenea hadi milele; ni rahisi kufokasi kwenye hapa na sasa na kusahau ya baadaye.

Nilifundishwa somo hili kwa nguvu miaka kadhaa iliyopita na binti yetu Jenifa aliyekuwa na miaka 16 wakati huo. Alikuwa karibu kupandikizwa mapafu mawili, ambapo sehemu tano zenye ugonjwa za mapafu yake zingeondolewa kabisa na nafasi yake kuchukuliwa na sehemu mbili ndogo zenye afya, zilizotolewa na marafiki wawili wazuri wenye sifa za urafiki kama wa Kristo. Ilikuwa ni upasuaji hatari sana, lakini usiku uliotangulia upasuaji wake, Jennifer alinihubiria mimi kwa takribani pauni zake zote 90, (41 kg) akisema, “Usijali, Baba! Kesho nitaamka na mapafu mapya au nitaamkia mahali bora zaidi. Vyo vyote iwavyo itakuwa vizuri.” Hiyo ndiyo imani; huo ndiyo mtazamo wa milele! Kuyaona maisha kutoka katika nafasi ya milele kunatoa uwazi, faraja, ujasiri na matumaini.

Baada ya upasuaji, siku iliyokuwa ikingojewa kwa muda mrefu ilipofika ya kutoa bomba la kupumulia na kuzima kifaa cha upumuaji ambacho kilikuwa kikimsaidia Jennifer kupumua, tulingoja kwa hamu kuona ikiwa sehemu zake mbili ndogo zingefanya kazi. Aliposhusha pumzi yake ya kwanza, papo hapo akaanza kulia. Alipoona wasiwasi wetu, alisema upesi, “Ni vizuri sana kupumua.” 

Tangu siku hiyo, nimemshukuru Baba wa Mbinguni asubuhi na usiku kwa uwezo wangu wa kupumua. Tumezungukwa na baraka zisizohesabika ambazo tunaweza kuzichukulia kirahisi kama hatutakuwa waangalifu. Kinyume chake, wakati hakuna kitu kinachotarajiwa na kila kitu kinathaminiwa, maisha huwa ya ajabu.

Rais Nelson amesema: “Kila asubuhi mpya ni zawadi kutoka kwa Mungu. Hata hewa tunayovuta ni mkopo wa upendo kutoka Kwake. Anatuhifadhi siku baada ya siku na kututegemeza kutoka wakati mmoja hadi mwingine. Kwa hivyo, tendo letu la kwanza la asubuhi linapaswa kuwa sala ya unyenyekevu ya shukrani.”13

Hiyo inanileta kwenye uchunguzi wangu wa tano na wa mwisho, ambao ni kwamba hutawahi kuwa na furaha zaidi kuliko unavyoshukuru.

Bwana alitangaza, “Na yule apokeaye vitu kwa shukrani atatukuzwa.”14 Labda hii ni kwa sababu shukrani huzaa wingi wa fadhila zingine.

Jinsi gani ufahamu wetu ungebadilika ikiwa kila asubuhi tungeamka na baraka ambazo tulikuwa na shukrani kwazo usiku uliopita. Kukosa kuthamini baraka zetu kunaweza kuleta hali ya kutoridhika, ambayo inaweza kutunyima shangwe na furaha ambayo shukrani huleta. Wale walio katika jengo kubwa na pana hutushawishi kutazama zaidi ya alama, na hivyo kuikosa alama kabisa.

Katika uhalisia, furaha kuu na baraka za maisha ya duniani zitapatikana katika kile tulichokuwa kupitia neema ya Mungu tunapofanya na kushika maagano matakatifu pamoja Naye. Mwokozi wetu atatusafisha na kututakasa kupitia sifa za dhabihu Yake ya kulipia dhambi na amesema kuhusu wale wanaomfuata kwa hiari, “Watakuwa wangu katika siku ile nitakapokuja kufanya vito vyangu.”15

Ninakuahidi kwamba ikiwa tutajenga maisha yetu juu ya msingi wa Yesu Kristo; kuthamini utambulisho wetu wa kweli kama wana na binti za Mungu; kukumbuka thamani ya nafsi; kudumisha mtazamo wa milele; na kwa shukrani kuthamini baraka zetu nyingi, hasa mwaliko wa Kristo wa kuja Kwake, tunaweza kupata furaha ya kweli tunayotafuta wakati wa uzoefu huu wa maisha ya duniani. Maisha bado yatakuwa na changamoto zake, lakini tutaweza kukabiliana vyema na kila moja kwa kusudi na amani kwa sababu ya kweli za milele tunazozielewa na kuishi kwazo.

Ninatoa ushuhuda wangu wa utakatifu na uhalisia wa Mungu, Baba yetu mwenye upendo, na Mwanawe mpendwa, Yesu Kristo. Pia ninashuhudia kuhusu manabii walio hai, waonaji na wafunuzi. Ni baraka iliyoje kupokea ushauri wa mbinguni kupitia wao. Kama vile Mwokozi alivyosema kwa uwazi, “Iwe ni kwa sauti yangu mwenyewe au kwa sauti ya watumishi wangu, yote ni sawa.”16 Katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina.

Chapisha