Liahona
Kichwa cha habari: Matangazo Mubashara ya Mkutano Mkuu kwa Mara ya Kwanza Ethiopia
Septemba 2024


Kurasa za Karibu

Kichwa cha habari: Matangazo Mubashara ya Mkutano Mkuu kwa Mara ya Kwanza Ethiopia

Watakatifu wa Ethiopia na Wakazi Wamekuwa na Matangazo Mubashara ya Mkutano Mkuu kwa Mara ya Kwanza, Kubarikiwa kwa Watakatifu, na Kubarikiwa kwa Nchi.

Siku ya mfungo inayokaribia Mkutano Mkuu wa Oktoba 2024 itakuwa mara ya pili katika historia kwamba Mkutano Mkuu utarushwa mubashara katika nchi ya Ethiopia. Aprili 2024 ilikuwa Mkutano wa kwanza kuwahi kurushwa kwa umma huko Ethiopia.

Baadhi ya waumini wa kanisa nchini Ethiopia waliulizwa kile ilichomaanisha kuwa na Mkutano Mkuu kurushwa mubashara katika nchi yao. Kwa kuwa kanisa ni changa, wale wote walioshiriki ni waongofu kanisani. Kila mmoja ana hadithi ya kustaajabisha ya jinsi walivyokuja kwenye Kanisa lililorejeshwa la YesuKristo.

Waongofu wapya Gemechu Feyissa na mwanaye Betselot Gemechu, ambao wote wamejiunga na Kanisa mwaka uliopita, walikuwa na furaha kujifunza kumhusu Yesu na kuwa na wenzao Waethiopia wakiangalia Mkutano Mkuu. “Watu wa Ethiopia wanapenda kuangalia TV,” Gemechu alisema. “Belageru ni chaneli maarufu. Watu wengi wataona Mkutano Mkuu.”Gamechu alituma mialiko ya kuangalia Mkutano Mkuu kwa majina 250 ya WhatsApp yake.

Atsede Demissie Arega alikuwa na ndoto miaka 20 iliyopita ambazo zilimleta Kanisani. Kabla ya kujiunga na Kanisa, alikuwa akijiuliza, “Mungu yuko wapi?” Alimpata Mungu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Alieleza kuwa kabla ya Aprili 2024, aliweza kuona vikao vya Mkutano Mkuu wiki kadhaa baadaye kwenye jengo la Tawi lake la kanisa, sasa anaweza kutazama Mkutano Mkuu mubashara akiwa nyumbani kwake. “Nina shukrani kubwa,” alisema, “ninahisi kwamba Mungu anaiona Ethiopia.” Aliwaalika wamisionari wa tawi lake kuja nyumbani kwake kutazama Mkutano Mkuu. Aliwaalika pia majirani zake waje na kutazama au watazame katika nyumba zao.

Kupata kijitabu cha Urejesho kikiwa chini mtaani huko Addis Ababa, Ethiopia kulimwongoza Zerge Weld Mariam kutafuta na kujiunga na Kanisa la YesuKristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho miaka 15 iliyopita. Kijitabu kilikuwa kimechapishwa katika lugha ya Amharic, lugha mama ya Ethiopia na kilikuwa na namba ya simu juu yake. Baada ya kusoma kijitabu na kumhisi “roho mzuri,” alipiga namba ile. Kwa mmisionari aliyepokea simu, Zerge alisema, “Nahitaji kujiunga na kanisa hili.”Familia yake ilimfuata kwenye uumini wa kanisa. Miaka kumi iliyopita, Zerge alikuwa na wakati mgumu katika maisha yake. Sabini Mkuu mwenye Mamlaka Mzee Edward Dube alikwenda nyumbani kwake na kumpatia baraka. Baada ya hilo, maisha yake yalibarikiwa, alikuwa na chakula cha kula na majaribu yake yalifanywa kuwa mepesi. Alipenda kuweza kuinua mkono wake wa kuume na kumkubali Mzee Dube, na viongozi wengine wa kanisa, wakati alipotazama Mkutano Mkuu mubashara katika nyumba yake, kwa mara ya kwanza.

Dada Yeweinshet Bezu Biru ni mwanamke wa kustaajabisha. Yeye na binti yake Helaina ni waumini waliojitoa wa kanisa na waliojitoa kuwapenda na kuwatumikia majirani zao. Dada Biru anatatizo la uoni. Anawapa makazi na matunzo wasichana 16 wa umri wa balehe. Shirika la Utah based Stirling Foundation hutoa msaada wa kifedha ulio muhimu kwa ajili ya makazi na matunzo ya wasichana 16. Dada Biru na Heleina, sambamba na wasichana wao 16, walifurahia pamoja kikao cha Jumamosi asubuhi cha Mkutano Mkuu. Walipata msisimko kuweza kuinua mikono yao ya kuume kumkubali Rais Russell M. Nelson sambamba na waumini wa kanisa ulimwenguni kote. Dada Biru alishiriki kwamba muumini mmoja wa tawi lake hakuwa na TV, hivyo alikwenda kwenye nyumba ya jirani asiye muumini na kutazama pamoja nao. Alilirudia hilo kwa matangazo mubashara ya Jumapili asubuhi.

Rais Kefeni Tesfaye Anbesse, Mshauri wa pili katika Urais wa Kanisa wa Wilaya ya Addis Ababa, mkewe Helina Tsega Tesema na watoto wao 3, walikuwa na shukrani kuweza kutazama vikao viwili vya Mkutano Mkuu mubashara kwenye nyumba yao. Waliwaalika pia marafiki waweke Belageru TV ili kusikia maneno ya manabii, waonaji na wafunuzi kwa siku mbili mnamo Aprili.

“Ninahisi kwamba Mungu anaiona Ethiopia,” alisema Atsede Demissie Arega, wakati akizungumza kuhusu matangazo ya kihistoria ya Mkutano Mkuu huko Ethiopia. Hakika, anaiona.