2023
Ukarimu kwenye Jukwa
Machi 2023


“Ukarimu kwenye Jukwa,” Rafiki, Machi. 2023, 28-29.

Ukarimu kwenye Jukwa

Damien alitamani asingemfokea dada yake.

Picha
Msichana mdogo akiendesha farasi kwenye jukwa huku ameshikilia fimbo

Wakati Damien alipoingia kwenye eneo la mchezo, alisikia muziki wa furaha ukichezwa. Bibi yake alikuwa amewapeleka yeye na dada yake mdogo, Adele, kuendesha jukwa yake aipendayo. Ilikuwa ni mchezo wa kuburudisha. Damien alihamasika kumwonyesha Adele jinsi ya kuucheza.

Punde wakawa sambamba. Jukwa ilikuwa kubwa na yenye rangi nyingi, pamoja na farasi wadogo wengi wa kuchongwa. Watoto wenye tabasamu walikuwa juu ya farasi hao na walipunga mikono wakati wanaendesha.

“Kama utamshika farasi kwenye ncha, unaweza kucheza mchezo wa mviringo!” Damien alimwambia Adele. “Unaona fimbo ambazo watoto wamezishika? Na unamwona yule mtu aliyeshika ile miviringo?”

Damien alimwonyesha mfanyakazi. Mfanyakazi alikuwa amesimama karibu na ile jukwa huku ameshikilia mviringo. Walipokuwa wakiendesha juu ya jukwa, wale watoto walikuwa wakijaribu kuingiza fimbo zao kwenye mviringo ili kuichukua. Kila wakati walipochukua mviringo, mfanyakazi aliwaonyesha mwingine mpya.

Adele alipiga makofi. “Ninataka kukamata miviringo yote!” alisema.

Mwishowe walifika mbele ya mstari. Lakini palikuwa na farasi mmoja tu aliyebaki kwenye jukwa hiyo.

“Damien,” Bibi alisema, “kwa nini tusimwache Adele achukue nafasi hii ya mwisho kwa vile yeye hajawahi kuendesha jukwa? Wewe unaweza kuendesha zamu inayofuata?

“Sawa,” Damien alijibu kwa kunung’unika. Alimwangalia yule mfanyakazi akimsaidia Adele kupanda juu ya yule farasi wa rangi ya kahawia. Kisha mfanyakazi yule akampatia Adele fimbo ya kukamatia miviringo.

Muziki ukaanza, na ile jukwa ikaanza kuzunguka. Damien alimwangalia Adele kutoka upande ule pamoja na Bibi. Lakini Adele alishikilia ile fimbo kwa nyuma! Badala ya kushikilia fimbo kwenye mshikio mkubwa, yeye alishika mwisho mrefu, mwembamba unaotumika kudaka miviringo.

Picha
Mvulana akipiga kelele

“Adele, geuza fimbo yako!” alipiga kelele. Lakini Adele alionekana kutomsikia kutokana na kelele. Wakati anaupita mviringo, fimbo yake ikaugusa. Lakini mshikio ulikuwa mkubwa sana kuweza kuingia ndani ya mviringo.

“Adele, fimbo yako!” Damien alijaribu tena. “Wewe hutaweza kukamata mviringo kama unashika fimbo namna hiyo!”

Lakini Adele hakumsikia? Yeye alitabasamu na kucheka wakati jukwa ilipokuwa inazunguka. Fimbo yake iligusa mviringo tena na tena. Hakukamata hata mviringo moja.

Damien aliguna. Adele alikuwa anapoteza zamu yake! Kama yeye angekuwa kwenye jukwa, angekamata miviringo yote.

Mzunguko ulivyoisha, alimkimbilia Adele.

“Nilikuambia namna ya kushika hii fimbo!” alisema kwa sauti. “Kwa nini hukunisikiliza mimi? Ulifanya makosa!”

Adele hakumpigia makelele Damien. Hakulia. Yeye alisimama tuli na alionekena mdogo, mdogo, mdogo.

Moyo wa Damien ulidunda kwa nguvu, na uso ukawa mwekundu. Ilimfanya akasirike kumwangalia Adele akiikosa miviringo ile yote. Lakini ilikuwa ni mara yake ya kwanza tu. Hata hivyo, ilionekana kwamba alifurahia mchezo. Hadi sasa.

Damien alijihisi vibaya sana. Damien alitamani asingemfokea dada yake.

“Samahani,” alisema kwa upole. “Sijakufanyia vizuri.”

Adele alitazama juu.

“Unaonaje kama mimi ningekupatia baadhi ya vidokezo kuhusu kukamata miviringo?” Damien alisema. “Mimi nitakaa nyuma yako kwenye jukwa na nitakusaidia.”

Adele aliitikia kwa kutikisa kichwa.

Picha
Dada na Kaka wakishikana mikono

Kisha Damien akamgeukia Bibi. “Tunaweza kupata tiketi mbili ili Adele aweze kujaribu tena?”

Bibi alitabasamu. “Bila shaka!”

Hadithi hii ilitokea huko Ufaransa.

Picha
PDF ya hadithi

Vielelezo na Violet Lemay

Chapisha