2023
Yesu Kristo Alibatizwa
Machi 2023


“Yesu Kristo Alibatizwa,” Rafiki, Machi. 2023, 24-25.

Hadithi za Yesu

Yesu Kristo Alibatizwa

Ondoa kurasa hizi na uzikunje katikati. Kisha shika picha na iinue juu huku ukisimulia hadithi hiyo.

Picha
picha ya kuchora ya Yesu akiwa anabatizwa na Yohana Mbatizaji

Picha hii na Greg Olsen

Yohana Mbatizaji alikuwa nabii. Alifundisha watu kuhusu Yesu Kristo. Siku moja Yohana alikuwa akibatiza watu katika Mto Yordani. Basi Yesu alimjia. Alimwomba Yohana Ambatize.

Yesu alisema Baba wa Mbinguni ameamuru kila mtu abatizwe. Yeye alitaka kumtii Baba wa Mbinguni. Yeye alitaka kuweka mfano kwa ajili yetu.

Yohana akambatiza Yesu katika Mto Yordani. Yesu alipotoka majini, watu walisikia sauti ya Baba wa Mbinguni. Akisema, “Huyu ni Mwanangu mpendwa, ninayependezwa naye.”

Tunaweza kumfuata Yesu Kristo kwa kubatizwa. Baba wa Mbinguni Anafurahi tunapomfuata Mwanawe.

Chapisha