“Sala ya Tetemeko la Ardhi,” Rafiki, Machi. 2022, 4–5.
Sala ya Tetemeko la Ardhi
Violet alipoamka, kila kitu kilikuwa kinatikisika.
Hadithi hii ilitokea huko Peru.
Violet alikuwa amelala wakati sauti ya mtetemo ilipomwamsha. Mwanzoni, yeye alidhani ni radi.
Lakini mtetemo uliendelea zaidi na zaidi. Ilitikisa madirisha ya chumba chake cha kulala.
Violet akakaa kitako kwa haraka. Hili lilikuwa tetemeko la ardhi.
Yeye na familia yake walikuwa wamehamia tu Peru sio muda mrefu. Alijua kuwa matetemeko ya ardhi mara kwa mara yanatokea hapa. Na yeye na familia yake walikuwa wamejiandaa na kufanyia mazoezi ya kile cha kufanya. Lakini hili lilikuwa la kutisha zaidi kuliko alivyodhania. Aliweza kuhisi mwili wake ukitetemeka.
Violet alikimbilia jikoni na kujikunyata chini ya meza. Sekunde chache baadaye, kaka yake na dada yake wakaungana naye. Vivyo hivyo Mama na Baba.
“Kazi nzuri mmekumbuka kile tulichokifanyia mazoezi,” alisema Baba. “Je, kila mtu yuko SAWA?”
Kaka na dada yake Violet waliitika kwa kichwa.
Lakini Violet alikuwa anaogopa. Yeye alifumba macho yake. Ilikuwa vigumu kudharau mtetemo uliomzunguka.
Kisha Violet akakumbuka kusali. Akakunja mikono yake na kuinamisha kichwa chake. “Mpendwa Baba wa Mbinguni,” alinong’ona, “tafadhali ilinde familia yangu.”
Violet aliendelea kusali. Alihisi kama mtu alikuwa anampatia kumbatio. Alipomaliza, aliangalia juu. Mama na Baba walikuwa wamekunja mikono yao. Kaka yake na dada yake nao walifanya vivyo hivyo. Wote walikuwa wakisali! Ardhi bado ilikuwa inatikisika. Lakini Violet alihisi amani moyoni na akilini mwake.
Mwishowe, mtikisiko ulikoma. Violet na familia yake waliendelea kukaa chini ya meza kwa muda kidogo, ili kuwa salama zaidi.
“Je, unahisije?” Mama alimwuliza Violet.
“Niko SAWA,” Violet akasema. “Mwanzoni nilikuwa nimeogopa sana. Lakini kusali kumenisaidia nihisi vizuri zaidi.” Violet akampa Mama kumbatio. Alikuwa na furaha kwamba Baba wa Mbinguni alikuwa amemsaidia ahisi amani.