Shughuli za “Njoo, Unifuate kwa Watoto Wadogo,” Rafiki, Machi. 2023, 49.
Agano Jipya
Shughuli zaNjoo, Unifuate kwa ajili ya Watoto Wadogo
Kwa ajili ya Mathayo 8; Marko 2–4; Luka 7
Ni mambo gani ambayo yanawaogopesha watoto wako wadogo? Kwa utulivu zungumzia mojawapo ya hofu zao. Kisha wasaidie kusema, “Ninapokuwa naogopa, Yesu anaweza kunisaidia nihisi amani.”
Kwa ajili ya Mathayo 9–10; Marko 5; Luka 9
Kusanya vifaa vya huduma ya kwanza na elezea jinsi vinavyotumika ili kutuponya sisi. Kisha elezea kwamba nguvu ya Yesu Kristo ya kuponya ni kubwa zaidi. Elezea moja ya miujiza katika Mathayo 9.
Kwa ajili ya Mathayo 11–12; Luka 11
Orodhesha siku za wiki kwa ajili ya watoto wadogo. Sema majina ya kila siku kwa sauti, lakini nong’ona unapotaja “Jumapili.” Eleza kwamba Jumapili ni siku maalumu ambayo kwa unyenyekevu hutufundisha kuhusu Yesu Kristo.
Kwa ajili ya Mathayo 13; Luka 8; 13
Elezea kwamba miaka mingi iliyopita, watu waaminifu walikuja kwa Yesu ili kusikiliza hadithi Zake (ona Mathayo 13). Waombe wachore picha ya watu wanamsikiliza Yesu.
Kwa ajili ya Mathayo 14; Marko 6; Yohana 5–6
Andaa vitafunwa vyenye afya kwa ajili ya watoto wenu wadogo. Simulia hadithi ya muujiza wa mikate na samaki (ona Mathayo 14:15–21). Wasaidie kusema, “Yesu anajua kitu ninachohitaji na anaweza kunisaidia.”