2023
Yesu Anatuliza Dhoruba
Machi 2023


“Yesu Kristo Akituliza Dhoruba,” Rafiki, Machi. 2023, 46-47.

Hadithi za Maandiko

Yesu Anatuliza Dhoruba

Picha
Yesu akiwa amelala kwenye mashua wanafunzi Wake wanaangalia bahari

Vielelezo na Apryl Stott

Usiku mmoja Yesu na wanafunzi Wake walivuka bahari kwenye mashua. Yesu alikuwa amechoka na akalala.

Picha
Dhoruba iliisukasuka mashua iliyokuwa na Yesu pamoja na wanafunzi Wake

Mara tufani ilikuja. Mawimbi yakawa makubwa zaidi na zaidi! Wanafunzi waliogopa. Walimwamsha Yesu na kumwomba awaokoe.

Picha
Yesu akiituliza bahari

Yesu alisimama na kusema, “Nyamaza, utulie. Tufani ilikoma. Maji yakatulia.

Picha
Mvulana mdogo amekunja mikono yake na macho yake ameyafumba.

Imani yangu katika Yesu Kristo inaweza kuniletea amani. Wakati ninapoogopa, Yesu anaweza kunisaidia nihisi amani.

Chapisha