2023
Amani kutoka kwa Mwokozi
Machi 2023


“Amani kutoka kwa Mwokozi,” Rafiki, Machi. 2023, 2-3.

Kutoka Urais wa Kwanza

Amani kutoka kwa Mwokozi

Imetoholewa kutoka “Amani katika Maisha Haya,” Liahona, Des. 2016.

Wasichana wawili na mvulana wachukua sakramenti

Vielelezo na Dilleen Marsh

Mwokozi alisema, “Ulimwenguni mnayo dhiki” (Yohana 16:33). Hiyo inamaanisha kwamba duniani sisi sote tutakuwa na nyakati ngumu. Lakini pia Yeye alitupatia sisi ahadi: “Amani nawaachieni, amani yangu nawapa” (Yohana 14:27). Kwa kumfuata Mwokozi, tunaweza kuhisi amani katika nyakati ngumu.

Tunapochukua sakramenti, sisi tunaahidi daima kumkumbuka Mwokozi. Unaweza kufikiria kuhusu Yeye katika njia ambazo zinakusaidia wewe kuhisi uko karibu Naye. Nyakati zingine ninamfikiria Yeye akiwa amepiga magoti katika Bustani ya Gethsemane. Nyakati zingine ninapata picha ya Yeye akimwita Lazaro atoke kaburini. Nifanyapo hivyo, ninahisi kuwa karibia Naye. Ninahisi shukrani na amani. Na wewe unaweza pia.

Yesu aliahidi kwamba tunaposhika amri Zake na kumfuata Yeye, Roho Mtakatifu atakuwa pamoja nasi. Ndipo tunapoweza kupata amani, bila kujali kile kinachotokea katika maisha yetu.

Hadithi za Yesu

Ukurasa wa kupaka rangi wa Yesu Kristo akisali katika bustani.

Rais Eyring alisema anahisi mwenye shukrani na amani anapofikiria kuhusu Mwokozi katika Gethsemane. Ni hadithi gani za Yesu zinazokusaidia wewe kuhisi uko karibu na Yeye?