2023
Kimbia kuelekea Nuru
Machi 2023


“Kimbia kuelekea Nuru,” Rafiki, Machi. 2023, 32—33.

Rafiki kwa Rafiki

Kimbia kuelekea Nuru

Imetoholewa kutoka “Running toward the Light” (video), ChurchofJesusChrist.org.

Picha
Mvulana anakimbia akiwa amevaa begi la mgongoni

Kielelezo na Adam Nickel

Nimekulia katika sehemu hatari ya jiji kubwa. Siku moja nilikuwa nikitembea kuelekea shuleni nikiwa na pesa katika mfuko wangu. Sarafu zilikuwa zikilia wakati nikitembea.

Ilinihitajika kutembea kuwapita baadhi ya wavulana wakubwa ambao ni genge la wahuni. Nilijaribu kuonekana kama ninajiamini. Nilijaribu kutokuogopa. Lakini walisikia mlio ule wa sarafu. Walitaka zile sarafu na kuanza kunifukuza.

Nilikimbia haraka kadiri nilivyoweza ili kuwaponyoka. Niliingia kichochoroni. Niliweza kuona mwangaza mwisho wa kile kichochoro, hivyo nilikimbia kuelekea kwenye ule mwanga. Punde wakaacha kunifuata, na nikawa salama.

Huu ukawa mpangilio katika maisha yangu. Nilikimbia kutoka kwa kilichokuwa kibaya, na nilikitafuta kile kilichokuwa kizuri. Nyakati zingine nilikatishwa tamaa, lakini nilijaribu kutafuta nuru.

Nilipokwenda chuo, nilicheza katika timu ya mpira wa kikapu. Wengi wa wana timu wenzangu walikuwa waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Nilijifunza kuhusu injili kutoka kwao. Nilijifunza kwamba mimi ni mwana wa Mungu. Hiyo ilimaanisha kwamba ningeweza kuinuka juu ya mahangaiko yangu na kuwa bora zaidi. Nikajiunga na Kanisa. Tangu wakati huo, nimejaribu kila siku kuwa zaidi kama Bab yangu wa Mbinguni na Mwanawe, Yesu Kristo. Na wewe unaweza kufanya hivyo pia.

Unapokimbia kuelekea kwenye mwanga, kuna matumaini. Unajua kuwa unakimbilia kwenye nguvu, amani na furaha. Sisi sote tunahitaji kukimbilia kwenye nuru.

Burudani ya Mpira wa Kikapu

Picha
Shughuli ya kumkwepa adui kwenye mpira wa kikapu

Mzee Johnson alijifunza kuhusu injili wakati akicheza mpira wa kikapu. Sasa ni zamu yako!

  1. Kata na miraba ya hapo chini na uikunjekunje kuwa mipira.

  2. Fanyeni zamu kuitupa iingie ndani ya bakuli.

  3. Mpira unapotua ndani ya bakuli, fungua hiyo karatasi na ujibu swali lake!

  • Ni njia gani moja ambayo unaweza kumfuata Baba wa Mbinguni?

  • Ni lini wewe ulichagua lililo sahihi?

  • Ni kwa jinsi gani wewe unaona nuru ya Baba wa Mbinguni katika maisha yako?

  • Je, ni kitu gani kinakusaidia wewe uhisi upendo wa Baba wa Mbinguni?

  • Ni kwa jinsi gani wewe unaweza kushiriki nuru ya Baba wa Mbinguni na wengine?

  • Andika maswali yako wewe mwenyewe!

Chapisha