2023
Ni Lilian tu
Machi 2023


“Ni Lilian Tu,” Rafiki, Machi. 2023, 40-41.

Ni Lilian tu.

Lilian hakutaka kuwa peke yake katika darasa la Wasichana.

Picha
Msichana mwenye huzuni akiangalia nyuma yake

Leo ilikuwa siku ya mwisho kwa Lilian katika Msingi. Lilian angewakumbuka watoto wengine wa Msingi. Walikuwa watatu tu—wasichana wadogo wawili na kaka yake mdogo mmoja, Michael.

“Je, unahisije kuhusu kuhamia kwa Wasichana?” mwalimu wake wa Msingi alimuuliza.

“Siwezi kungojea kwenda kwa wasichana wakubwa!” Lilian alisema.

“Ninafurahia kuwa unayo shauku,” mwalimu wake alisema. Ni wakina nani watakuwa pamoja nawe kwenye kikundi cha Wasichana?

Lilian aliwafikiria wasichana wakubwa katika kata. Summer na Cova wamemaliza tu shule ya upili. Na familia ya Melvina wamehama. Ngoja. Hiyo ilimwacha . . . Lilian tu.

Je, darasa lake la Wasichana litakuwaje? Je itakuwa walimu tu na yeye? Hilo halikuwa jambo zuri—na la upweke. Akifikiria kuhusu hilo Lilian alipatwa na wasiwasi. Alikunja uso. Hakutaka kuwa mtu pekee katika Wasichana.

Kwa muda uliosalia kwa siku hiyo, Lilian aliendelea kufikiria juu ya kuwa msichana peke yake. Wakati wa chakula, yeye alikizungusha tu chakula kwenye sahani yake bila kula. Alimunyamunya ilipofika zamu yake kusoma wakati wa kujifunza maandiko.

Mama aliweka maandiko yake chini. “Nini kibaya?” aliuliza.

Lilian alishusha pumzi. “Ninakwenda kuwa pekee yangu katika darasa la Wasichana!”

Mama alisogea ili akae karibu na Lilian. Akampa kumbatio. “Hiyo haitakuwa rahisi,” alisema. “Tunaweza kufanya nini ili kumsaidia?”

Lilian alifikiria kwa muda mfupi. “Pengine tunaweza kusali ili msichana mwingine ahamie katika kata yetu. Na pengine Baba angeweza kunipatia baraka.”

Baba akatabasamu. “Hayo ni mawazo mazuri zaidi.”

Familia ilipiga magoti kusali. “Baba wa Mbinguni,” Lillian alianza, “Ninashukuru kuwa nahamia darasa la Wasichana. Sitaki kuwa pekee yangu, lakini kama hayo ni mapenzi yako, yote ni sawa. Tafadhali nisaidie kujua kile cha kufanya ili niweze kuhisi vyema. Na kama unataka kuishawishi familia yenye msichana wa umri wangu kuhamia katika kata yetu, hilo lingekuwa zuri pia.

Baada ya sala hiyo, Baba aliweka mikono yake juu ya kichwa chake. “Ninakubariki wewe kwamba utahisi amani kuhusu kuhamia darasa la Wasichana,” Baba alisema. “Baba wa Mbinguni atakubariki unapoomba msaada Wake.

Lillian alijihisi mwenye amani. Hakuwa na uhakika bado wa nini angefanya ili kuhamia darasa la Wasichana kuwe rahisi. Lakini pia alijua Baba wa Mbinguni angemsaidia.

Picha
Msichana akipata baraka

Jumapili, Lilian alikuwa bado mwenye wasiwasi. Lakini alikumbuka amani aliyohisi baada ya Baba kumpa baraka. Alijua kuwa atakuwa SAWA.

Katika mkutano wa sakramenti, askofu alitangaza kwamba Dada Barns angekuwa rais mpya wa Wasichana. Dada Barns alisimama jina lake lilipoitwa. Lilian hakuwa anamjua, lakini alionekana kuwa rafiki.

Mama alisema kwamba alipokuwa umri wa Lilian, kiongozi wao wa Wasichana alikuja kuwa rafiki yake mkubwa. Yawezekana Liliana na Dada Barns wangeweza kuwa marafiki! Hilo liilikuwa ndilo jibu la maombi yake.

Baada ya mkutano wa sakramenti, Lilian alienda kwenye darasa lake jipya. Msichana mkubwa alikuwa amesimama ndani ya ukumbi.

“Halo,” Lilian alisema. “Je, unatembelea kata yetu?”

Msichana alitikisa kichwa chake. “Hapana. Familia yetu imehamia tu hapa.”

Lilian alitabasamu. “Karibu katika kata yetu. Hii ni siku yangu ya kwanza katika darasa la Wasichana. Yeye na yule msichana wakakaa chini pale darasani. “Tuache hayo, jina langu ni Lilian.”

“Haiwezekani! yule msichana mgeni alisema. “Jina langu ni Lilian pia!”

Lilian alicheka. Baba wa Mbinguni alikuwa amejibu maombi yake tena. Yawezekana kuwepo katika darasa la Wasichana hakutakuwa na upweke kabisa.

Picha
Wasichana wawili wanaongea na wameshika maandiko

Hadithi hii ilitokea huko Australia.

Picha
PDF ya hadithi

Vielelezo na Sue Teodoro

Chapisha