“Shughuli za Njoo, Unifuate,” Rafiki, Machi. 2023, 6–7.
Shughuli za Njoo, Unifuate
Kwa ajili ya jioni ya nyumbani, kujifunza maandiko au burudani tu!
Dhoruba
Kwa ajili ya Mathayo 8; Marko 2–4; Luka 7
Hadithi: Soma hadithi ya Yesu Kristo akituliza dhoruba kwenye ukurasa wa 46 au katika Marko 4:36–41. Zungumzia kuhusu njia ambazo Yesu anakuletea wewe amani.
Wimbo: “I Feel My Savior’s Love” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 74–75)
Shughuli: Simameni katika mzunguko na kushika pembe za blanketi. Wekeni mpira juu ya blanketi na pole pole uzungusheni huku na huko, kama mashua ilivyosukwasukwa juu ya mawimbi. Peaneni zamu kuliambia kundi kwenda haraka, kupunguza mwendo au “tulia.”
Muujiza wa Kubashiri Mchezo
Kwa ajili ya Mathayo 9–10; Marko 5; Luka 9
Hadithi: Yesu Kristo alifanya miujiza mingi. Yesu alimponya mtu aliyekuwa hawezi kutembea. Alimrudishia uhai mtu aliyekuwa amekufa. Alimponya mtu aliyekuwa kipofu. (Ona Mathayo 9.) Ni miujiza gani mingine Yesu alifanya?
Wimbo: “Tell Me the Stories of Jesus” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 57)
Shughuli: Andika baadhi ya miujiza ya Yesu kwenye vipande vya karatasi na uviweke ndani ya bakuli. Okota karatasi, soma muujizi ulioandikwa na uchore picha yake. Wengine wanaweza kubashiri ni muujiza gani!
Kufanya Kazi Pamoja
Kwa ajili ya Mathayo 11–12; Luka 11
Hadithi: Yesu Kristo alisema, “Nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi” (Mathayo 11:30). Nira inawasaidia wanyama wawili kuvuta mzigo kwa pamoja. Tunapochagua kumfuata Yesu, Yeye anaweza kutusaidia sisi na majaribu yetu.
Wimbo: “If the Savior Stood Beside Me” (ChurchofJesusChrist.org)
Shughuli: Mwambie mtu auhamishe mzigo mzito aupeleke upande mwingine wa chumba. Kisha auhamishe kwa kusaidiana na mtu mwingine. Zungumza kuhusu jinsi mizigo yetu inavyokuwa miepesi zaidi tunapo mgeukia Mwokozi kwa ajili ya kupata msaada.
Andika Mfano Wako Mwenyewe!
Kwa ajili ya Mathayo 13; Luka 8; 13
Hadithi: Yesu alifundisha injili kwa kutumia hadithi zinazoitwa “mifano.” Hadithi moja Yeye aliyosema ilikuwa ni kuhusu jinsi gani mbegu ndogo ya haradali inavyoweza kukua na kuwa mti mkubwa (ona Mathayo 13:31–32). Yeye alikuwa anafundisha nini? Ni mifano gani mingine Yesu alifundisha?
Wimbo: “If I Listen with My Heart” (ChurchofJesusChrist.org)
Shughuli: Mifano inaweza kutusaidia sisi kuelewa injili vizuri zaidi. Geuza ukurasa wa 8 ili kuandika mfano wako mwenyewe. Shiriki mfano wako na washiriki wa familia au marafiki.
Zaidi ya Kutosha
Kwa ajili ya Mathayo 14; Marko 6; Yohana 5–6
Hadithi: Wakati mmoja Yesu Kristo alitumia siku nzima akiwafundisha watu. Kila mmoja alikuwa na njaa. Lakini walikuwa na mikate mitano na samaki wawili tu. Yesu akabariki mkate na samaki na wanafunzi wake wakaigawa kwa watu. Palikuwako na chakula cha kutosha zaidi ya watu 5,000! (Ona Mathayo 14:15–21).
Wimbo: “I’m Trying to Be like Jesus” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 78–79)
Shughuli: Tengeneza mapishi yako pendwa ya mkate au jaribu yaliyoko kwenye ukurasa wa 8. Tambua jinsi kitu kidogo kama hamira kinavyoweza kufanya mkate kuwa mkubwa zaidi. Ni kwa jinsi gani Yesu Kristo amefanya jitihada yako ndogo kuwa kitu kikubwa?