2023
Siku Yangu ya Ubatizo
Machi 2023


“Siku Yangu ya Ubatizo,” Rafiki, Machi. 2023, 12–13.

Imeandikwa na Wewe

Siku Yangu ya Ubatizo Wangu

Picha
Familia na wasichana watatu wakienda kanisani

Habari! Jina langu ni Mergan, na ninaishi Mexico. Ninataka kukuambia kuhusu wakati maalumu sana katika maisha yangu—siku niliyobatizwa.

Nilibatizwa kwenye siku yangu ya miaka nane ya kuzaliwa. Ilikuwa siku yangu muhimu sana kwa sababu nilisherehekea siku ya kuzaliwa kwangu kwa kubatizwa.

Kubatizwa lilikuwa tukio zuri sana. Mama yangu alinitengenezea daftari lenye shughuli tofauti tofauti ili kujiandaa. Lilinisaidia mimi kujifunza kuhusu umuhimu wa ubatizo na maagano ambayo ningefanya na Baba wa Mbinguni.

Picha
Msichana aliyevaa gauni la waridi ameshika daftari

Watu wengi wanaonipenda walikuja kwenye ubatizo wangu. Nilihisi furaha sana kwamba walikuja. Nilivaa gauni jeupe, na maji yalikuwa ya uvuguvugu.

Baada ya baba yangu kunibatiza, nilijikausha na kubadilisha nguo. Kisha nikapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. Nilithibitishwa kuwa muumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho na wenye ukuhani. Nilijihisi mwenye amani, upendo na furaha tele.

Picha
Msichana akibatizwa wakati watoto wengine wanaangalia.

Daima nitaikumbuka siku ile. Ilikuwa maalumu sana kwa sababu nilifanya agano langu la kwanza na Mungu. Niliahidi kumfuata Yesu na kutii amri Zake.

Picha
Msichana akimkumbatia baba

Kama una wasiwasi kuhusu siku yako ya ubatizo itakuwaje, usihofu. Baba wa Mbinguni atakuwa na furaha kuhusu uchaguzi uliofanya.

Picha
PDF ya hadithi

Vielelezo na Olga Lee

Chapisha